Naomba msaada anaefaham dawa nzuri ya kuongeza damu kwa mtoto

mmongoro

Member
Mar 31, 2019
66
51
Habari za usiku na poleni na uchovu wa weekend naomba mwenye kufahamu tiba nzuri ya kuongeza damu kwa kutumia dawa za asili anisaidie ninachomaanisha sio dawa za Hospitalini. Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna yale majani yanaitwa mashona nguo.Majani flani hivi ukipita mbegu zake kama sindano zinanata kwenye nguo zako.
Chukua majani yake twanga ongeza maji kamua kunywa kikombe cha chai asubuhi mchana na jioni baada ya wiki kapime wekundu wa damu yaani HB kisha rudi JF lete ripoti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna yale majani yanaitwa mashona nguo.Majani flani hivi ukipita yakakugusa mbegu zake kama sindano zinagusa.
Chukua majani yake twanga ongeza maji kamua kunywa kikombe cha chai asubuhi mchana na jioni baada ya wiki kapime wekundu wa damu yaani HB kisha rudi JF lete ripoti

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukur sn changamoto dar sijawahi kuyaona haya majani lkn kwa mkoani nimewah kusikia habari hizi za majani haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mtoto wa umri gani na uliambiwa damu imepungua kwa sababu gani? Ukijua kilichosababisha damu ikapungua ndio inakuwa rahisi kukupa ushauri, kwa mfano kama mwanao ana sickle cell lishe hutaweza kuongeza damu kwa vyakula!
 
Beetroots zitasaidia sana, kama mtoto ni mkubwa na ana uwezo wa kutafuna mwenyewe mkatie katie atafune, ila kama ni msumbufu hawezi kutafuna mwenyewe fanya kumsagia kama juice umpatie anywe.
 
Nilibahatika kufanya research katika majani ya viazi ( wanaita tembele) plus beetroots l, matokeo yakaja positive kwa ongezeko la blood related factor kama vile PCV, Hb, RBCs...

Wewe cha kufanya anza kutengeneza juice ya tembele na Beetroots anza kunywa kila siku asubuhi mchana na jioni damu itaongezeka kwa wingi mkuu....

Pia tembelea jaribu kuzila kwa sana kama mbogamboga...
 
Back
Top Bottom