Naomba mnishauri niombe course gani NACTE?

Naomba mnishauri niombe course gani NACTE?

Wewe sasa hivi tafuta pesa uje usome engineering diploma.tena nenda mechanical. Serikali yetu haiitaji walimu ....kwanini unajitafutia maisha ya tabu kila siku?

haha!nashukuru mkuu kwa ushauri wako.
 
Habari wana JF
Naomba ushauri kutoka kwenu waungwana;
Nilimaliza kidato cha IV mwaka 2011 na kufanikiwa kupata alama ambazo ni za kawaida kama ifuatavyo:
Basic Mathematics-C
Chemistry-B
Engineering Science-C
Kiswahili-C
English Language-C
Civics-C
Geography-D
Surveying-C
Building Construction-D
Architectural Draughting-D
Ambayo ni Division II ya pointi 20 Na nikachaguliwa kwenda kidato cha V mwaka 2012 mchepuo wa PCM shule moja iliyokuwa na mchanganyiko wa O-level(Day)
na A-level(Boarding).

Shule ilikuwa ndio inachukuwa A-level kwa mara ya kwanza na ilichukuwa wanafunzi wa michepuo ya Sayansi tupu ambayo ni PCB,CBG na PCM jambo la kusikitisha ilikuwa haina mwalimu wa A-level hata mmoja.

Na wanafunzi tulishauriwa na mkuu wa shule kwamba "Anayetaka kuhama Ruksa"
Na mimi nilikuwa sina mtu wa kunitafutia uhamisho nikaomba ruhusu ya wiki 2 na kuanza mchakato wa kutafuta shule,nilizunguka sana mpaka mkuu wa shule mojawapo akanihisi nimharifu na kutishia kuniitia Polisi kwa sababu namsumbua.Nilichanganyikiwa sana.

Nikasitisha kwa muda na kurudi shule lakini likizo ya mwezi Disemba mwaka 2012 nikaendelea kutafuta na mwishowe mwezi Februari 2013 nikapata nafasi kwenye shule nyingine nakupewa OPTIONS, aidha nianze kusoma mwezi huo mpaka itakapoanza likizo ya muda mrefu kuhitimisha kidato cha V lakini kwa kulipa gharama zote za kidato cha tano ambayo ilikuwa kama 252,000 pamoja na michango au nijiunge muhula uliofuata mwezi Julai na kuanza kidato cha VI.

Kwa sababu sikuweza kumudu gharama hizo nikaomba kuchukua Option namba
mbili.
Baada ya hapo nikarudi shuleni kupewa kibali cha kufuatilia uhamisho mkoani,mwishowe nikamaliza taratibu zote na muhula mpya ulipoanza nikahamia shule husika lakini walimu wa shule hiyo walikuwa wamemaliza kufundisha topics zote hivyo walikuwa wakifanya REVISIONS tu,hali ilikuwa mbaya kwa upande wangu lakini sikukata tamaa ingawa ilibaki miezi 10 kufanya mtihani wa Taifa.

Mwezi MEI mwaka 2014 nikafanya mtihani na sikufanikiwa kufaulu kwani nilipata alama hafifu kama ifuatavyo:

General Studies-D
Physics-D
Adv.Maths-E
Chemistry-E
Na mwaka huo ndio GPA ilianza kutumika,hivyo sikufanikiwa kwenda
popote.
Na ilipotangazwa Diploma maalum ya Ualimu pale UDOM kipindi hicho nilikuwa natumikia Jeshi la Kujenga Taifa hivyo taarifa sikuzipata mpaka nilipomaliza mafunzo DISEMBA 2014 na kurudi mtaani.

Nikajaribu kukusanya pesa ili angalau niweze kurudia mtihani mwaka huu lakini gharama zake zilikuwa kubwa kwa sababu masomo yangu yanahitaji PRACTICALS,Gharama ya Kituo niliambiwa 80,000,Mtihani 65,000.

Na topic nyingi za Sayansi ni gharama kubwa kwani zipo zinazofikia mpaka 45,000 na TOPIC zipo zaidi ya 20 hivyo nikagonga mwamba kwa mara nyingine.
Nimejaribu kutafuta vyuo vya afya nakutana na kigezo cha somo la BIOLOGY ambalo
mimi nililisoma mpaka kidato cha pili tu kwa sababu ya Limit kwenye masomo ya
kufanyia mtihani ambayo ni 10.

Sasa,naomba ushauri kwenu ni kozi ipi naweza kuichukua kwa vigezo hivyo vya ufaulu wa kidato cha nne;siku ambayo
NACTE watafungua maombi.
Upishi...
 
Miaka 6. Na unadhani mtu wa diploma akitoka hawezi kazi au? Huyo miakka mitatu tu anaenda kutafuta ajira.
ushasahau bongo bila degree🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
 
ushasahau bongo bila degree🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
Acha kasumba degree kitu gani. Engineering haiangalii degree au diploma linapokuja swala la kazi as teamwork. Hapa namaanisha kuwa degree sio sababu
 
Acha kasumba degree kitu gani. Engineering haiangalii degree au diploma linapokuja swala la kazi as teamwork. Hapa namaanisha kuwa degree sio sababu
ok kak nimekuelewa nyie na fan za sayans waiobak bila degree pasua kichwa
 
Duh pole sana huwa nasikitika sana nikisikia mtu ndoto zake zimekwama sababu ya kukosa hela tena hela ndogo kiasi hicho huwa naumia sana ila yote ni mipango ya mungu usijali riziki yako ipo ...mi sina ushauri ila nmependa watu walivyokushauri usome mambo ya ardhi au civil au engineering mungu atakusaidia ..ardhi wana chuo tabora kama unayo ada nenda nacte ukajielezee wakupangie chuo direct kama hapo juu walivyokushauri pole sana nimeumia
 
Duh pole sana huwa nasikitika sana nikisikia mtu ndoto zake zimekwama sababu ya kukosa hela tena hela ndogo kiasi hicho huwa naumia sana ila yote ni mipango ya mungu usijali riziki yako ipo ...mi sina ushauri ila nmependa watu walivyokushauri usome mambo ya ardhi au civil au engineering mungu atakusaidia ..ardhi wana chuo tabora kama unayo ada nenda nacte ukajielezee wakupangie chuo direct kama hapo juu walivyokushauri pole sana nimeumia

asante kwa ushauri wako.Samahani utakuwa unajua ada ya hicho chuo?
 
Samahani,Je,nikiomba kujiunga na Dar-es-salaam Institute of Technology(DIT) nitapata fursa ya kuwa Government-sponsored au la?kwa anayejua tafadhali anifahamishe ili hata kesho niende NACTE nikajieleze pengine naweza kusaidiwa!Inshaallah.
 
Mkuu upo wapi kwanza??? Anyway nenda ofisi za NACTE kanda waeleze shida yako na Sababu zilizokufanya uchelewe kuomba uende Chuo sahv Maana kuanzia mwakani kama ulimaliza Form 4 kuanzia 2011 kurudi nyuma hutaweza kupata Chuo cha serikali
 
kwa mazingira ya Tanzania na maabara zetu kusomea engineering ni tatizo
Wanaosomea IT wote hawaishii kuwa bloggers, kuna ambao wapo na career nzuri tu, na Dunia sasa inabadilika mambo mengi yanabadilika kutokakwenye manual kwenda computerized system, so ni industry inayokuwa
Dah! We jamaa utakuwa huangalii mbali.
 
Mimi nipo Dar lakini tatizo sujajua ada zao!

Na vipi kuna ukweli wowote kuhusu kutopata vyuo vya serikali mwaka kesho?
 
Back
Top Bottom