Naomba mnishauri niombe course gani NACTE?

Naomba mnishauri niombe course gani NACTE?

Korozoni

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2016
Posts
264
Reaction score
106
Habari wana JF
Naomba ushauri kutoka kwenu waungwana;
Nilimaliza kidato cha IV mwaka 2011 na kufanikiwa kupata alama ambazo ni za kawaida kama ifuatavyo:
Basic Mathematics-C
Chemistry-B
Engineering Science-C
Kiswahili-C
English Language-C
Civics-C
Geography-D
Surveying-C
Building Construction-D
Architectural Draughting-D
Ambayo ni Division II ya pointi 20 Na nikachaguliwa kwenda kidato cha V mwaka 2012 mchepuo wa PCM shule moja iliyokuwa na mchanganyiko wa O-level(Day)
na A-level(Boarding).

Shule ilikuwa ndio inachukuwa A-level kwa mara ya kwanza na ilichukuwa wanafunzi wa michepuo ya Sayansi tupu ambayo ni PCB,CBG na PCM jambo la kusikitisha ilikuwa haina mwalimu wa A-level hata mmoja.

Na wanafunzi tulishauriwa na mkuu wa shule kwamba "Anayetaka kuhama Ruksa"
Na mimi nilikuwa sina mtu wa kunitafutia uhamisho nikaomba ruhusu ya wiki 2 na kuanza mchakato wa kutafuta shule,nilizunguka sana mpaka mkuu wa shule mojawapo akanihisi nimharifu na kutishia kuniitia Polisi kwa sababu namsumbua.Nilichanganyikiwa sana.

Nikasitisha kwa muda na kurudi shule lakini likizo ya mwezi Disemba mwaka 2012 nikaendelea kutafuta na mwishowe mwezi Februari 2013 nikapata nafasi kwenye shule nyingine nakupewa OPTIONS, aidha nianze kusoma mwezi huo mpaka itakapoanza likizo ya muda mrefu kuhitimisha kidato cha V lakini kwa kulipa gharama zote za kidato cha tano ambayo ilikuwa kama 252,000 pamoja na michango au nijiunge muhula uliofuata mwezi Julai na kuanza kidato cha VI.

Kwa sababu sikuweza kumudu gharama hizo nikaomba kuchukua Option namba
mbili.
Baada ya hapo nikarudi shuleni kupewa kibali cha kufuatilia uhamisho mkoani,mwishowe nikamaliza taratibu zote na muhula mpya ulipoanza nikahamia shule husika lakini walimu wa shule hiyo walikuwa wamemaliza kufundisha topics zote hivyo walikuwa wakifanya REVISIONS tu,hali ilikuwa mbaya kwa upande wangu lakini sikukata tamaa ingawa ilibaki miezi 10 kufanya mtihani wa Taifa.

Mwezi MEI mwaka 2014 nikafanya mtihani na sikufanikiwa kufaulu kwani nilipata alama hafifu kama ifuatavyo:

General Studies-D
Physics-D
Adv.Maths-E
Chemistry-E
Na mwaka huo ndio GPA ilianza kutumika,hivyo sikufanikiwa kwenda
popote.
Na ilipotangazwa Diploma maalum ya Ualimu pale UDOM kipindi hicho nilikuwa natumikia Jeshi la Kujenga Taifa hivyo taarifa sikuzipata mpaka nilipomaliza mafunzo DISEMBA 2014 na kurudi mtaani.

Nikajaribu kukusanya pesa ili angalau niweze kurudia mtihani mwaka huu lakini gharama zake zilikuwa kubwa kwa sababu masomo yangu yanahitaji PRACTICALS,Gharama ya Kituo niliambiwa 80,000,Mtihani 65,000.

Na topic nyingi za Sayansi ni gharama kubwa kwani zipo zinazofikia mpaka 45,000 na TOPIC zipo zaidi ya 20 hivyo nikagonga mwamba kwa mara nyingine.
Nimejaribu kutafuta vyuo vya afya nakutana na kigezo cha somo la BIOLOGY ambalo
mimi nililisoma mpaka kidato cha pili tu kwa sababu ya Limit kwenye masomo ya
kufanyia mtihani ambayo ni 10.

Sasa,naomba ushauri kwenu ni kozi ipi naweza kuichukua kwa vigezo hivyo vya ufaulu wa kidato cha nne;siku ambayo
NACTE watafungua maombi.
 
Kwa hayo matokeo yako hukuwa na vigezo mwaka huu?
Anyway, inaonekana unapenda sayansi ila kwa Tanzania ya sasa, sijui mbeleni kutakuaje sikushauri ukasome engineering chuo ni kazi ngumu ambayo haiendani na return utakazopata na kujiajiri pia ni ngumu
Pengine ungejaribu kusomea IT kama unapendezwa nayo, ni nzuri na nisekta inayokua kwa kasi, na kama wewe unapenda na unaweza kujiajiri ukijituma..kila la kheri
 
Mkuu wewe ni engineering tu. Ulisoma shule maalum ya ufundi. Kwa ufaulu wako kila diploma ya engineering unasoma. Kazi kwako kujipanga. Tafta pesa soma mwakani . Mwaka huu samehe tu mkuu.
 
Kwa hayo matokeo yako hukuwa na vigezo mwaka huu?
Anyway, inaonekana unapenda sayansi ila kwa Tanzania ya sasa, sijui mbeleni kutakuaje sikushauri ukasome engineering chuo ni kazi ngumu ambayo haiendani na return utakazopata na kujiajiri pia ni ngumu
Pengine ungejaribu kusomea IT kama unapendezwa nayo, ni nzuri na nisekta inayokua kwa kasi, na kama wewe unapenda na unaweza kujiajiri ukijituma..kila la kheri

Acha kupotosha. Asisomee engineering vipi sasa? Mbona unamtoa mwenzio ktk sehemu ya kueleweka unampeleka matatizoni. Unajua soko la IT lilivyo? Unataka aishie kuwa blogger?
 
Acha kupotosha. Asisomee engineering vipi sasa? Mbona unamtoa mwenzio ktk sehemu ya kueleweka unampeleka matatizoni. Unajua soko la IT lilivyo? Unataka aishie kuwa blogger?
kwa mazingira ya Tanzania na maabara zetu kusomea engineering ni tatizo
Wanaosomea IT wote hawaishii kuwa bloggers, kuna ambao wapo na career nzuri tu, na Dunia sasa inabadilika mambo mengi yanabadilika kutokakwenye manual kwenda computerized system, so ni industry inayokuwa
 
Fanya mpango mwakani uende Engineering DIT au ATC
 
I don't know, ila kwa mazingira ya Tanzania na maabara zetu kusomea engineering ni tatizo
Wanaosomea IT wote hawaishii kuwa bloggers, kuna ambao wapo na career nzuri tu, na Dunia sasa inabadilika mambo mengi yanabadilika kutokakwenye manual kwenda computerized system, so ni industry inayokuwa
You don't KNOW. If you don't know you have no right to speak. Hapa tuangalie uhalisia wa bongo this era. Jamaa akasome engineering. Kuliko kupoteza muda na IT. Aangalie electrical au mechanical. Wapi ana interest napo akasome. Otherwise atarudi tena huyu kuja hapa jukwaanii
 
Aisee pole sana, ila natamani siku zingerudi nyumba, wakati zinatakiwa hizo 252,000 wakati wa
kuanza form V Ungekuja hapa japo kuomba msaada, ukachangiwa, chukua huo ushauri wa kusubiri mwakani tena kujiunga na chuo kama hali bado ni tete.
 
yamefungwa ila ukiwaelezea sababu za kuchelewa una pewa chuo ndugu na tcu ni hvo hvo kuna barua unapewa kwamba ukaoneshe kuwa uko selected kwenye chuo x
Oooh ok...Asante kwa kunifahamisha.
 
ukifanikiwa ulete mrejesho......
Sio mimi ila nina mtu ndo nilimwambia atafute chuo akaja kunijibu kwa sasa maombi yameshafungwa. ila nitamshauri hivyo akifanikiwa nitakuja wafahamisha.
 
Aisee pole sana, ila natamani siku zingerudi nyumba, wakati zinatakiwa hizo 252,000 wakati wa
kuanza form V Ungekuja hapa japo kuomba msaada, ukachangiwa, chukua huo ushauri wa kusubiri mwakani tena kujiunga na chuo kama hali bado ni tete.

ndio hivyo tena!inaumiza sana but no way!
 
yamefungwa ila ukiwaelezea sababu za kuchelewa una pewa chuo ndugu na tcu ni hvo hvo kuna barua unapewa kwamba ukaoneshe kuwa uko selected kwenye chuo x

Dah!ngoja nisubiri mwakani tu!sasa hivi niendelee kuhangaikia gharama!
 
Back
Top Bottom