Naomba mawazo yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba mawazo yenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Edson, Dec 14, 2009.

 1. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  naomba mnisaidie mawazo ndugu zangu. niliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja wa kichaga, nilipokuwa chuo mwaka wa pili yeye alikuwa ndo alijiunga mwaka wa kwanza ila mahusiano yetu yalianza mbali kama miaka miwili kabla ya yeye kuingia chuo.ilifikia kipindi ikabidi tuweke mambo wazi mbele ya wazazi, ndugu na jamaa pia.

  nilipomaliza chuo nilipata nafasi ya kwenda nje kusoma kozi ya mwaka mmoja. niliacha kila kitu huku nyumbani kiko sawa, mimi na mchumba wangu huyu kulikuwa hakuna shida yoyote, ikizingatiwa kuwa pande zote mbili zilikuwa zinafahamu juu ya uhusiano wetu. nikiwa huko nje nasoma, mawasiliano yalikuwepo tena mazuri tu.

  miezi kama saba ilipopita kukawa na matatizo lakini sikujua chanzo ni nini maana kila nilipokuwa napiga simu akawaanaongea kwa mkato sana tofauti na mwanzo, nikimuuliza mbona uko hivyo? anajibu kwani nikoje? basi kwa kuwa nilikuwana upendo wa dhati sikupenda saana kumkwaza.ndugu zake pia niliwasiliana nao. kuna siku moja nilimpigia simu mchumba wangu akasema amekwenda kumtembelea rafiki yake kwao na kuna kipindi niliwahi kuongea na rafiki yake na akasema wako rikizo so wametembeleana.

  Mungu alinisaidia nikasoma nikamaliza salama kozi yangu. nikarejea nyumban salama, huyu mchumba wangu alikuwa chuo ndo anamalizia, nilipofika hatukuweza kuonanana maana aliniambia mitihani iko karibu na pia test zipo kibao so anajiandaa, niliheshimu mawazo yake nikaenda mwanza kwa wazazi wangu kuwajulia hali. nikiwa huko nyumbani nilipata ujumbe toka kwa rafiki yake kuwa mchumba wangu ni mjamzito na mgonjwa sana hajiwezi. nikapigwa na butwaa sana.habari zikafika kwa ndugu zake nao wakaenda dar kumchukua na kwenda nae moshi.nami nikaelekea huko kumwona mgonjwa. daktari akasema ujauzito umeharibika na ni wa mapacha kwa hiyo solution ni kuitoa mimba ili kunusuru maisha ya mama mjamzito. ujauzito ulikuwa wa miezi 6.

  daktari akasema ili tuitoe mimba tunahitaji sahihi ya baba aliyempa binti huyu ujauzito, binti akaulizwa muhusika yuko wapi akasema hayupo karibu akasema yuko dodoma.mda wote nilikuwa nimekaa kimya tu .baada ya mda kukawa na majadiliano ndugu zake wakaja kwangu wakaniambia niweke sahihi. nikawauliza kama nani maana sie niliyempa ujauzito. wakanisihi sana baada kama ya dk 20 nikaambiwa mgonjwa ananiita ndani , nilipofika akaniambia '' please naomba uokoe maisha yangu, naomba uweke sahihi'' nikapiga moyo konde, ndugu zangu wana jf niliweka sahihi, mimba ikatolewa.
  baada ya kulazwa kwa mda hosp baada ya mda akatolewa hosp.nikataka kujua nini kilimpelekea akanisaliti kiasi hicho, hakuwa na la kusema zaidi ya kusema nisamehe shetan alinipitia.ndugu zake walinisihi nisibadili uamuzi wangu, ndugu zangu waligawanyika.
  kwa kuwa nilikuwa nampenda sana nilisamehe kila kitu na nikasau yaliyotokea. ikiwa imebaki miezi mitatu amalie chuo, nilimvisha pete ya uchumba, mbele ya wazazi wangu na wazazi wake na ndugu wengine .mda ukapita ikiwa tumekubaliana tufunge ndoa mwezi wa 12. mahali nikalipa ila sikumaliza yote.

  kila kitu kikiwa sawana nikisubiri siku ya tukio ifike, ilikuwa ni tarehe 12/9/2006 majira ya saa kumi jioni nilipokea ujumbe mzito toka kwa huyu mchumba wangu ulisomeka hivi '' nimekaa na kutafakari kwa kina na kuona kuwa wewe si mwanaume wa maisha yangu, samahani kwa yote naomba utafute mtu mwingine atakaye kufaa mimi na wewe hatuendani''
  nilipoisoma sms ile nilichanganyikiwa sana, nikampa mdogo wangu akausoma nikamwambie wafowadie wazazi wake na pia wazaz wetu huko mwanza.familia ya kwao na binti ilikaa, wakamwita binti akasafiri, mimi niliambiwa nisiende huko siku ya kikao. nikatii. kwenye kikao binti alishka msimamo wake huo kuwa hanitaki, mama yake mzazi alipojaribu kumsihi na kumuuliza binti yake; biti alimjibu hivi nama yake mzazi '' kama unataka kuolewa wewe olewa mimi siolewi na wala usinilazimishe eti kwa ababu ni mama yangu''. nilipopata taarifa hii nilifunga safari hadi kwao na binti na nikaelezwa hayo, mama yake na binti alipata na mshituko wa moyo akalazwa hosp.
  niliwashukuru wote kwa jitihada zao, nikawaambia kuwa hili ni somo tosha nimelipata. nilimtumia binti sms ya kumtakia maisha mema lakini mwisho niliandika kuwa ''MANENO HUUMBA''
  nilikata tamaa ya maisha hasa kuoa sikuona faida tena, nikaomba nafasi ya kwend nje kusoma masters ili walau niondoke huku tanzania, nikafanikiwa nikapata.nimesoma huko denmark,mwaka 2007 mwishoni nilipata bint mmoja wa kipoland, akanipenda,kabla penzi halijawa zito nikamsimulia kisa hiki ili ajue yaliyonisibu.penzi likawa penzi. tukajaaliwa tukapata mtoto mmoja wa kike anaitwa Blanca. mwaka jana mwezi wa nane tumefunga ndoa. na ninaishi na mke wangu huyu mama blanca mpaka leo.

  sasa ndugu zangu wana jf kilichonisukuma nikaomba ushauri na mawazo yenu ni kwamba huyu dada aliyenitosa amekwenda kwa wazazi wangu kuwaomba radhi anasema eti toka aachane na mimi maisha yake ni mabaya sana,kila anachojaribu kufanya kinashindkana japo ana kazi nzuri, anawaambia wazaz wangu wamuombee msamaha,na ikibidi nimuoe.wazaz wakamwambie kwa mimi nimeshaoa na nina mke na mtoto. mpaka dakika hii ninayoandika hapa huyu binti yuko nyumba kwetu mwanza anasubiri tamko toka kwangu. nimewauliza wazaz hana kazi wamesema ameomba likizo. jana nimempigia mama simu na kumwambia kuwa sina msamaha wowote ila aende kwao akamuobe baba yake radhi kwa kusababisa kifo cha mama yake mzazi maana mama yake alikufa kutokana na maradhi ya moyo ambaye yeye ndo alikuwa chanzo pale alipomwambia mama yake kuwa kama unataka kuolewa olewa wewe.
  mpaka sasa yuko kwetu pale sengerema hataki kuondoka wazaz wangu wamemwelewesha lakni dada haelewi, ndugu zangu nipeni mawazo nifanyeje ili atoke pale kwetu. tarehe 19 naanza likizo na nitaondoka nchini kwenda poland ukweni kwa ajili ya mapumziko na kumpeleka mwanangu kuwaona babu ba bibi yake.

  nasubiri msaada wenu.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Pole sana kamanda Edson, mimi sioni cha wewe kuomba ushauri hapa umetoswa mara mbili mkuu na huyo binti, tayari umeoa na upo happy na wife wako na mna mtoto. Achana na huyo opportunist atakuharibia maisha yakoo mzee, utaishia kuwa na frustration bureee hawa mabinti wa kichaga bana siku hizi hawashikiki tena, they are very after MONEY!
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pole sana kwa yaliyo kukuta,ingawa na mm nimesalitiwa pia tena leo lkn sikufikia stage ya mchumba,nakushauri mpigie huyo mchumba wako wa zamani simu,mwambie unaomba aondoke kwenu maana ni mzigo ktk familia yenu pia hamna undugu wowote sasa iweje anakaa kwenu,so unamuomba aondoke kwenu tena haraka sana,maana huna mahusiano nae yoyote.
   
 4. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  we shika zako hamsini...alikutesa na kukudhulumu siku yake imefika anajuta...plus u seem like a very kind lovable man...married and happy achana nae akae akichoka ataondoka!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  japo kaambiwa una mke na mtoto kwasasa hajaridhika?....sasa uiache familia yako umouoe yeye, huyu kapoteza uelekeo kabisa......
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Edson, wat goes around comes around!! kinachompata anakistahili kabisa. analaana ya mama yake huyo, kwanza mshukuru Mungu alikuepusha mengi, huyo asingekuwa mke mwema kabisa!!! Kumtukana mama yake mzazi tusi la nguoni kama hilo?? No wonder alikusaliti!!!

  Nakusifu kwa moyo wa kusamehe na kukubali kuokoa maisha yake lakini kwa sasa, achana nae!! let her pay for what she did to you (na wazazi)

  Endelea kufurahia maisha yako na familia yako, no turning back. mwache akae kwenu likizo ikiisha arudi kibaruani!!!

  Enjoy your holiday Edson!!!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Once beaten, twice shy.... you had a shameful two experiences na huyo dada; wew mhakikishie umemsamehe [na umsamehe kikweli], halafu endelea na maisha yako... Yeye ni mkatili na huhitaji mtu wa namna hiyo kwani umeshaanza njia nyeupe ya maisha yako

  Mpe pole, mpe msamaha na mtakie kila la heri

  La mwisho nakuomba uwaeleze wazazi wako kwamba wasimkaribishe tena kwani atakuharibia na penzi lako jipya, hakuna mwananke atakayetolerate ex kuja kwenu kwa namna yoyote ile
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  You have said it well MTM
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  asante sana kwa ushauri
   
 10. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huyo dada nafikiri ana matindio wa ubongo. mwache akae sengerema ale nanasi ndiyo msimu wake. Ila tu ninachokuomba ibilisi huyu aliyeko kwenu kama ulikuwa na mpango wa kuja tanzania this month ahirisha, oportunist huyo ataharibu.

  La pili kwenu wasiendekeze mpumbavu, wampeleke polisi la sivyo wamchape makofi aende kwao pale siyo kwao.

  Amenichefua sana huyo dada! hana aibu hata moja kha!
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  nilishamsamehe kikweli kaka ila kwa hili la kuja ketu ndo nalitafutia njia hapa jf
   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  waambie wazazi wako wasimuintertain hapo kwenu kabisa tena atoe shombo lake hapo.

  au wamwache awasaidei kazi za nyumbani housegirl/boy naye apate kupumua for the time being!!!

  ana bahati mi si dadako!!!!!!!
   
 13. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  we bht mbona unatishia sana....ungekuwa ushamzaba makofi akaondoka bila kwaheri!!!
   
 14. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,031
  Trophy Points: 280
  We una bahati? Du yu knoo woram seeyyying?
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  yaani Shishi kama ulikuwepo!!! Ningemtoa 'nishai'!!!
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280

  kuna mdogo wangu nae amenipa ushauri kama huu kuwa nimtwagie baba simu then nimwambie wamuondoe hapo. dada yangu wa pekee edina yuko masomoni. kwanza hata mimi sitaki kuonana nae
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaa sasa shemeji kwa taarifa nataka niongee na Edson kama naweza kuwa his 'acting' sisy!!!
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,031
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Na ulivokuwa baunsa naona ungeua kabisa! Mungu apitishe mbali hiyo zahma!
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Niambie niact badala ya Edina aone cha moto huyo mwanamke katili!!!
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaaa mpwa/shemeji wewe bwana, yaani angeomba aangukiwe na nyumba!!
   
Loading...