Uwezekano huo upo kwa maana ya kwamba ni jambo ambalo lipo na limewekewa utaratibu kabisa wa hatua za kufuata ili kulikamilisha. Lakini sio lazima ukubaliwe/ufanikiwe, bado ni 50/50.
Swali langu kwako ni hili, bado huu ni wakati wa applications, ni kwanini usipate muda mzuri wa kutafakari na kupata ushauri ili uwe na kozi hata mbili au tatu ambazo kati ya hizo ukichaguliwa yoyote uwe tayari kuisoma na kuepusha michakato ya kuhamahama yenye usumbufu mwingi ?