Ndugu nlkuwa naomba tofauti kati ya memory na storage.
Halafu kwa nn App moja kwenye RAM na storage ya simu moja inakuwa na MB tofauti.
Natanguliza shukran wakuu
Storage pia ni memory, chochote kinachohifadhi kumbukumbu ni memory,
Ram yenyewe inahifadhi kumbukumbu lakini Ukizima kifaa inafuta kila kitu, na Storage inahifadhi kumbukumbu pia lakini Ukizima kifaa bado inahifadhi.
App moja kuwa na size tofauti inategemea na matumizi. Mfano mimi na wewe wote tunatumia whatsapp,
mimi natumia picha 100 kwa siku, nachat na watu 1000, natumia nyimbo na mambo kibao pamoja na kupokea.
Wewe kwa siku unachat na watu wawili tu maybe picha moja kwa wiki.
Hapa whatsapp yangu itakuwa na mb nyingi sababu inahifadhi backup ya chat zote, kutakuwa na thumbnail, na data nyengine.
Kuelewa zaidi nenda setting kwenye simu then apps tafuta app moja fungua nenda kwenye storage utaona wamegawanya mambo matatu. Actual size ya app, app data na cache, hizo app data na cache zinatokana na matumizi yako wewe hivyo zinafanya app moja kwenye simu mbili kuwa na size tofauti.