Naomba kujuzwa majani yanayofaa kwa ajili ya kujifukizia

Habari naomba kujuzwa Ni majani gani yanatumika kujifukiza kwa ajili ya hili janga.
Mkuu wahenga walishasema mficha maradhi kifo humuumbua....haya anza na majani ya mwarobaini,kisha utafute ya mpera.

NB: usichanganye majani katika mvusho mmoja.
 
Wewe endelea kufanya mzaha na maisha yako!Kumbuka binadamu huwa haishi mara mbili kwa hiyo nakushauri acha kufanya mzaha na maisha yako.Hizo dawa za kujifukizia zimejaribiwa wapi na lini zikaonyesha mafanikio?
 
Wazee wetu zamani walikuwa wakitumia hizo njia
Wazee wetu zamani waliugua Corona?Halafu hujajibu swali langu la msingi:Nimekuuliza hii njia ya kujifukizia imejaribiwa wapi na lini ikaonyesha mafanikio?
 
Vitu vya Msingi ni hivi:-

1.Vaa Barakoa
2.Tumia "SANTAIZA"
3.Nawa Mikono kwa sabuni na Maji tiririka
4.Epuka Misongamano(Social Distancing).

Vya ziada,Tumia sana Malimao kwenye mboga ,Tumia chai ya tangawizi au mchai chai huwa vinaboost kinga ya mwili hivyo ni itakuwa rahisi kupambana na infection.
 
Back
Top Bottom