#COVID19 Naomba kujuzwa gharama za kutivu Covid-19

Naomba kujua gharama za matibabu ya corona kama kuna mwenye experience kwa mfano dawa na sindano
 
Kuna ndugu yangu amelazwa hapo KCMC dawa na sindano n mtihani. Sindano moja 330,000 zinatakiwa ,6 na Leo anachomwa ya 6. Piga 330,000×6=1,980,000 bado dawa. Mpaka sasa zimetumuka zaidi ya ,milioni 3 kwenye sindano na dawa na bado hajapona. Huku pia akipiga dose za kiasili.

Ukweli Corona gharama ni kubwa Sana. Ila sasa ukigusa hospital kama Aghakan na Hindmandal na Kairuki na nyingine kubwa ndiyo utaimba nyimbo zote kama huna pesa.

Inatakuwa uweke deposit ya pesa ndefu huku ukitumwa ukanunue sindano na dawa na wanakuagizia Pharmacy maalum zinapopatikana. Nahisi ni biashara Yao pia. Corona nayo imetumika kama kitega uchumi kwa hospital binafsi
 
Aisee,Mwenyez Mungu awaponye kwa kweli.Kumbe kweli Tz IPO ee
 
Kuna ndugu yangu amelazwa hapo KCMC dawa na sindano n mtihani. Sindano moja 330,000 zinatakiwa ,6 na Leo anachomwa ya 6. Piga 330,000×6=1,980,000 bado dawa. Mpaka sasa zimetumuka zaidi ya ,milioni 3 kwenye sindano na dawa na bado hajapona. Huku pia akipiga dose za kiasili...
Propagandist
 
Propagandist
Hongera sana mkuu. Siku Corona ikikatiza kwenye familia yako au kwa mtu wako wa karibu nafikiri utatafakari mara mbili. Tunamshukuru Mungu ndugu yetu KCMC Oxygen ilikuwa 40 kwa sasa iko zaidi ya 80.

Mungu ni mwaminifu kwetu. Waendelee kupumzika kwa amani shangazi zangu wawili waliotangulia kwa Covid 2020 na 2021. Daaah yaani hakika huu ugojwa ni usikie kwa mtu na ukiamua kubeza kama wewe ni hiari tu. Lakini sisi ambao tumeshaguswa tuache tu.
 
Baba yangu ameshafariki anyway
Pole sana kaka mkubwa, jipe moyo mkuu.

Amini ni Mungu ameruhusu litokee jambo hilo,

Kumbuka kila nafsi itaonja umauti hata mimi na wewe siku yetu inakuja.

Mwenyezi Mungu awe faraja kwako na wote mliopatwa na msiba.

Raha ya milele u mpe ee bwana na mwanga wa milele umuagazie apumzike kwa amani.
 
Asanteni sana wakuu.. hali inatisha tujitahidi sana kuchukua tahadhari
 
Back
Top Bottom