Naomba kujua tofauti ya filamu na tamthilia

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
Kwa mwenye uzoefu naomba anitofautishie kati ya filamu na tamthilia especially za kitanzania.
 
kwa mwenye uzoefu naomba anitofautishie kati ya filamu na tamthilia especially za kitanzania
Za Tanzania haziwezi kuwa tofauti na misingi yake
Filamu huwa na ukomo wa hadithi ambao unaweza kuangalia maramoja na kumaliza
Tamthilia ukomo wa hadithi huhitaji vipindi kadhaa kuweza kufikia kikomo
 
Tofauti iliopo Ni filamu, imelenga katika kuburudisha zaidi, wakati tamthiria imelenga katika kufundisha. Mfano: Filamu Ili inoge, inahitaji iwe Na matendo mengi ya uwongo yasiyowezekana katika hali ya kawaida, ukweli uwepo kwa kiasi kidogo tu. Tamthia yenyewe imelenga katika kufundisha zaidi, inahitaji ukweli zaidi kuliko uwongo, hivo huigiza zaidi kwenye matendo ya kila siku yanayotokea kwenye jamii. Mpaka hapo nimekueleza vile ninavyojua tofauti, wajuzi watakuja na Maelezo zaidi.
 
Za Tanzania haziwezi kuwa tofauti na misingi yake
Filamu huwa na ukomo wa hadithi ambao unaweza kuangalia maramoja na kumaliza
Tamthilia ukomo wa hadithi huhitaji vipindi kadhaa kuweza kufikia kikomo
nashukuru mkuu kwa majibu,at least nimepata ka mwanga kidogo lakini bado sijaiva
 
Filamu inatakiwa iwe kazi inayoanza na kuisha ndani ya mda mfupi
hadithi isiwe na muendelezo

tamthilia inatakiwa kuwa hadithi ya kila wiki au kila siku
ambayo inaweza chukua miezi sita au hata miaka miwili au zaidi
 
Back
Top Bottom