Naomba kujua soko la Rupia ya Mjerumani na bei yake!

Naomba kujua soko la Rupia ya Mjerumani na bei yake!

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
4,700
Reaction score
1,090
Habari wadau!

Kuna ndugu yangu ana pesa ya zamani ya mjerumani maarufu kama rupia, sasa anataka kuuza! Je soko lake liko wapi na huwa zinauzwa kwa bei gani?

Naomba mtaalamu wa mambo hayo anijulish kwa PM.!

Nawasilisha
 
Habari wadau!

kuna ndugu yangu ana pesa ya zamani ya mjerumani maarufu kama rupia,sasa anataka kuuza! Je soko lake liko wapi na huwa zinauzwa kwa bei gani?

Naomba mtaalamu wa mambo hayo anijulish kwa PM.!

Nawasilisha

Hiyo biashara ni ya kusadikika nimeanza kusikia hadithi za rupia kuuzwa kwa mamilioni ya fedha tangu mwaka 1983 na juzi.

Kabla ya leo kuna mtu mmoja kanipigia simu anataka mteja wa rupia eti amekataa milioni 40 anataka zaidi ya hapo nilicheka sana nikamwambia kama hana kazi ya kufanya na simu yake bora aizime kuliko kuleta upuuzi huo, Rupia ni sawa na biashara ya albino mtu unadanganywa albino anauzwa milioni 600 unakwenda unamuua na unaanza kutafuta soko kumbe unakutana na polisi na wote waliouwa albino hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kupata fedha kwa kuwa ni maneno ya kijiweni.

Ukifuatilia hata huyo anayekuaminisha hajuia lolote la albino wala la hiyo rupia ni bora mkajikita kufanya kazi zinazoeleweka kuliko kukaa mnafikiria utajiri wa miujiza kwani mtabaki mnawaza mambo makubwa wakati hamna lolote hata chembe kwenye hizo hadithi za kusadikika na ni WASADIKIKIKA TU NDIYO WANAWEZA KUAMINI HAYO MAZINGAOMBWE YA KUUA ALBINO KUUZA RUPIA NA KUTAFUTA MAFUTA YA MSUKULE KWA CHUPA YA PPF KUUZWA MILIONI 600 UNAKUTA MTU HATA KAZINI AMECHOKA KWENDA AKIAMINI MUDA MFUPI UJAO ATAZINYAKA 600M KUMBE UJINGA MTUPU. Hiyo rupia iweke kama kumbukumbu ya wajukuuu zenu wewe na rafiki yako mtawaonyesha kuwa hiyo ilikuwa pesa ya mjerumani tu.
 
Alichosema BADO MMOJA ni kweli kabisa, hizi pamoja na ile hadithi ya eti Wajerumani waliacha mali nyingi ikiwa eti ni pamoja na almasi, dhahabu, zebaki nyekundu (Red Mercury) wakiwa eti wamefukia sehemu mbalimbali nchini ni HADITHI ZA KUSADIKIKA TU. Hata mimi nimeanza kusikia hadithi hizi kama miaka 20 iliyopita hivi lakini hadi leo sijaonyeshwa mtu mmoja aliyefanikiwa kwa hizo rupia au hizo hazina zilizofichwa. Jamani tufanye kazi tuachane na hizi BLAA BLAA.
 
Rupia , mayai ya Bundi etc. yanauzwa kiulagai sana, mtafute mtu muwe wawili, mmoja anatangaza soko ya rupia kwamba uko tayari kununua kwa milioni hata kumi then unaacha contact zako wakati wakiendelea kutafuta rupia inayohita(kwa specifications ulizotoa) then yule mwingine anjitokeza kwamba anazo(rupia)wakati huo wewe umeshaondoka eneo hilo. sasa wanaolizwa ni wale watakao ununua ili wakuuzie wewe, kwani utakua hupatikani tena. jihadhari na matapeli watakuliza
 
Who told u rupee was a Germany coin? Rupee comes from India, the Germans had Hella (so the name hela we usually use to denote fedha/pesa in Swahili).
Mythical stories, nothing like that.
 
Who told u rupee was a Germany coin? Rupee comes from India, the Germans had Hella (so the name hela we usually use to denote fedha/pesa in Swahili).Mythical stories, nothing like that.
Fatilia historia yako vizuri mkuu, Mjerumani alikuwa akitumia Repee pia na kuna baadhi zilikuwa zikitengenezwa Tabora
 
Achana na iyo biashara utakula za uso! yaan kama una gari utatembelea rim! wengi wamejaa utapeli ni biashara inayofanyika midomoni saana soko lake huji kuliona! Utapelekwa hotel zote za kitalii utaambiwa mzungu anayenunua kasafiri leo tuu!
 
Bilashaka ni full tapeli busnes(biashara tapeli)na kaka angu amekuakifanya biashara hiyo muda mrefu tangu 1972,na amekuwa akiifanya vijijini,pia amekuwa akifanya uganga wakitapeli na ramli tapeli,kama walivyo eleza mwingine anaweza tumia mzungu hewa. Inakuwa hivi kunamtu anakuja eneo lenu,vijiweni au kwenye maduka na viduka. Takriban wiki hadi mwezi anakuwepo eneo akitangaza na kuzoena na wafanya biasha ama mtu yoyote mwenye uhakika wakipato,aweza kuwa dereva bajaji,taksi nk, rupia anakua na zo yeye mwenyewe na anaweza mchukua kijana mtaani hapo akampa dili.kama dukani ataongena muuza duka na kumtaarifu bana kuna rupia zina hitajika ukiipata hii rupia ya1884 jerman ostafric iliyotengenezwa tabora nakupa milion tano au peleka mtu fulani au duka fulani kariakoo. We utakuwa na imani. Jamaa pengine atapotea sikumbil ama wiki atatokeza jamaa wahapo mtaani atakuletea na kukuuzi kama milioni sawa kama lakitano sawa itategemea makubaliano. Kama alikupa simu na dili limefanyika piga namba hiyo kama utaipata hewani piga piganawewe. Hapo umeliwa kama atakuwa hewani atakupa story nyingi nakwamba amepata matatizo yupo mbali naile biashara nayeye ametapeliwa. Sasa kama ganzi ya miguu inaanza kupanda ndo hivyo utaisoma
 
Ninazo rupia tofaut tofaut na pesa za zamani nyingi... Njoo na offer yako kwa PM
 
Back
Top Bottom