Naomba kujua kuhusu Kilindi Tanga

Naomba kujua kuhusu Kilindi Tanga

Benzoic

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
421
Reaction score
149
Wadau wa JF nimepata dili Kilindi Tanga lakini sijui mazingira ya huko yakoje. Mwenye nazo anijuze
NATANGULIZA SHUKRANI
 
kUNA MADINI SANA NASIKIA, JAPO BADO IKO MWITUNI SANA
 
kUNA MADINI SANA NASIKIA, JAPO BADO IKO MWITUNI SANA
Kuwa mwituni sana sio ishu sana kaka ...vipi huduma za muhimu kama usafiri, maji na makazi bora?
 
dili ni la muda mfupi au muda mrefu? Kupo poa tu ni kama zilivo wilaya changa zingine.
 
kilindi bdo hapajachangamka sana ila kuna ardhi yenye rutuba sana.
 
Tanzania hii hakuna sehemu mbaya kwa kuwa huduma zote muhimu zipo kila mahali. Nenda tu.
 
Mkuu kilindi kuko poa lkn bei ya chakula ipo juu sana pale wilayani Songe. Usafiri wa dar to kilindi upo ni Tsh.17,000/= maji ni ya kisima yana chumvi,umeme upo wilayani na miji iliyopo kando ya barabara itokayo Handeni to Songe, guest zipo nyingi hata za buku 2. Wenyeji ni Wazigua, Wanguu, Wamasai na Wakaguru. Uchawi hasa "tego" ni kitu cha kawaida. Kuna ardhi nzuri sana kwa kilimo, madini ya aina mbalimbali na misitu ya miti ya asili. Vipi dili lenyewe ni hapo wilayani songe au ni vijijini?
 
Back
Top Bottom