Naomba kujua kuhusu kauli ya Rais

acanthocyte

Senior Member
Nov 27, 2012
190
157
Wana JamiiForums salam.

Bila kupoteza muda naomba ufafanuzi kusuhu hii tafsiri kwamba Rais wa nchi akitamka kitu chochote inakuwa sheria au utekelezaji unaanza Mara moja bila kujali kama amekiuka katiba ya nchi au sheria zilizopo.

Sasa katiba yetu inasemaje juu ya matamshi ya Rais kuwa sheria?

Wajuzi wa sheria naomba ufafanuzi
 
Sio kila kauli ya rais ni sheria, bali zile kauli rasmi za rais zinazowekwa kwenye maandishi rasmi ya kirais, zenye mamlaka ya kirais ya kutunga sheria, ambazo zinatolewa kwa andishi rasmi la amri za rais zinazoitwa "presidential decree" ndizo sheria, ila pia sheria hizo lazima ziendane na katiba ya nchi, sheria yoyote itakayokwenda kinyume cha katiba, ni batili!.

Ila pia rais wa JMT, anayomadaraka makubwa sana ya kuweza kumfanya rais kuwa dikiteta wa ukweli kwa sheria zetu, mfano mzuri, ni japo bunge lina mamlaka ya kumshitaki rais na kumvua madaraka, "impeachment" lakini rais ana mamlaka ya kulivunja bunge!, ili kubwa kuliko, rais wetu, kama amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama, pia ana mamlaka ya kuiweka pembeni katiba, kwa kutangaza amri ya hali ya hatari, hivyo katiba kuwekwa pembeni, na nchi kuongozwa ama kijeshi, ama kwa amri kwa "presidential decrees!"

Wengi humu JF, Magufuli ndio wamemjua sasa baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM!, angalieni watu humu, walimjua lini, na walisema nini kumhusu!.

Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ..

Pasco
 
Ni Tanzania pekee ambapo ukisimamia sheria unaitwa Dikiteta...haya maajabu ya dunia.

Tanzania ni nchi ambayo inazo rasilimali nyingi ila haendeleo...tatizo ni mtu wa kusimamia taratibu na sheria zinazoongoza matumizi bora ya rasilimali hizo ili ziwanufaishe watanzania wote.

Sasa watanzania wamempata mtu sahihi wa kuwavusha wanamuita Dikitete aha!!!
 
MTU sahihi hawezi kubana democrasia, ninadhani MTU sahihi kwa upande wako na so kwa watanzania.
 
Rais kutamka neno kisha neno hilo kuwa sheria ni Sifa mojawapo ya Utawala wa kidikteta. "His will is the law" yaani utashi wake ndio sheria.
 
Back
Top Bottom