HabariHabari wana JamiiForums naomba msaada kwa yeyeto anaye jua gharama za matatibabu ya appendix
Asante mkuu nitafanya hivyoMkuu tembelea hospital mbili tatu zilizo karibu nawe.
Pole Sana.
Asante MkuuHabari
Pole kwa kuumwa.
Ni kweli kwamba matibabu kwa vituo vya afya gharama zake zinatofautiana sana.
Kutoka vile vya serikali na levels/kiwango cha kituo husika na daktari mhusika yaani qualifications. Na wapi walipo.
Lakini pia kwa vile vya private, levels ya kituo husika daktari mhusika na wapi kilipo.
Pia ni vyema kufahamu kuwa matibabu hutegemea na hali ya mgonjwa:
1: Kuna mgojwa daktari atamfanyia conservative management, yaani kumpatia dawa na kumwangalia atakavyoendelea hii ni kulingana na hali ya mgonjwa.
2: Kuna mgonjwa wa kufanyiwa operation kwaajili ya hiyo appendicitis.
3: Kuna mgonjwa mwenye appendicitis iliyokaa zaidi ya siku nne. Utaratibu wake unaweza kuwa tofauti kama itakuwa imefanya kitu kama jipu kubwa.
Kifupi itategemea wapi ulipo, kituo cha afya cha serikali au private, kiwango cha kituo, daktari husika na hali yako. Na kama kuna magonjwa mwambata kama sukari au pressure.
Matibabu mema.