Kuna aina mbili za watumiaji wa EFD. Wale ambao wamesajiliwa na VAT na wale ambao hawajasajiliwa na VAT. Wale ambao wamesajiliwa na VAT nao pia wanaweza kuwa wanauza bidhaa ambazo zinatozwa VAT na nyingine hazitozwi na VAT, setting yake inafanyika kwenye mashine. Lakini kwa wale ambao hawajasajiliwa na VAT wao wananunua bidhaa zao wanaongeza faida yao wanauza kwa kutoa risiti za EFD na mashine zao hazikati VAT. TRA wanachohitaji ni kupata uhalisia wa mauzo yako ili kuepusha ukadiriaji wa kodi usiokuwa na uthibitisho. Na hii inamsaidia mfanyabiashara kujua amenunua kiasi gani, ameuza kiasi gani na amepata faida kiasi gani, alafu akiondoa gharama nyingine kama umeme, maji, muuzaji, usafirishaji nk. Unapata faida halisi ambayo ndo kodi inatozwa hapo.