Naomba kufahamu ubora wa gari za Honda na engine zake

Barca

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,405
1,552
Habari za mida hii watalaam, mimi nimtumiaji wa magari gari yangu ya sasa ni Nadia engine 3s. Nina mpango wa kununua gari ambayo ina shape nzuri but cheap in price. Katika pitia mitandaoni nimependa sana shape ya Toyota harrier ila sasa ni expensive sana.

Nikaamua kubadili mawazo nikaanza shape inayofanana nayo. Katika pitapta nimeona HONDA CRV NA HRV. Naomba ushauri wa hizi gari mbili zipi ni nzuri kwa ubora wa engine na ukilinganisha mafundi wetu wa kuunga unga na spare parts.

Msaada kwenye tuta natanguliza shukrani.
 
Haina tatizo baada ya kumalizia series ya toyota land cruiser Vx ntaeleze Honda pia kwa hyo usiwaze tupo pamoja! ila samahan kwa kuwacheleweshea ombi lenu.
 
Nakushauri baki kwenye magari ya Toyota
Honda utalia spare zake labda km unaishi Miji mikubwa km Dar, Tanga au Arusha
km ni mtundu tafuta wataalam watakaokuwekea injini na gear-box za Toyota uweke kwenye hilo Bodi (usijenilaumu)
Ushauri wa mwisho ongezea ukaisakanye Harrier
 
nina honda crv mwaka wa 3 kimya kabisa na ninapiga ruti ndefu lkn gari haina shida yeyote kaaaabisa
 
Honda ni gari nzuri sana, nakumbuka ni my first car Honda Accord series ya mwaka 1985 yani ilikuwa inanizidi umri from the year of manufacture. Sasa kimbembe ni spare parts zake kama suspensions, engine parts na vinginevyo, kwa general service naona shida kwenye filters na aircleaners.
Ni gari inayivumulia mikikimikiki sana. kinachofanya iwe gharama kuihudumia ni Spares zake kutokupatikana maeneo mengi hapa nchini. Ila kwa CRV naona zipo nyingi tuu na parts zake zinapatikana pale ilala za kutosha sana, bei zake ni za kawaida hata vitz spare zake ni aghali kuliko hiyo CRV.

Kitu cha kuzingatia ,lazima ujue unanunua gari ajili ya matumizi gani. Usije nunua IST ukitegemea uipeleke shamba.
 
sio kweli nina crv mwaka wa 3 sasa na halina shida yeyote kaaabisa,tusipotoshe watu kwa kusikia tuuu maneno
 
wewe ushawahi kuwa nayo gari la honda usiropokwe toyota ndio mbovu ndio maana spare kibao kama hujui kwa maandishi hata picha huoni
 
hapana bhna wingi wa kitu sio ubovu wake , spea znakuja kulingana na mahtaj kuwa makubwa kutokana na magar husika kuwa mengi, kutokuona spea za aston martin huku co kwamba ni mazima sana ni kwamba hayapo hvo huez leta spea
 
Ni gari Nzuri mmmno,tena hi ni rd 1 la mwaka 1996,ukipata rd5 utainjoi mmmmno,hutajuta kamwe,ninalo ndo maana naongea
 
Back
Top Bottom