Naomba kufahamu kuhusu nchi ya Hungary!

Naomba kufahamu kuhusu nchi ya Hungary!

martial arts

Senior Member
Joined
Jun 26, 2014
Posts
191
Reaction score
100
Habarini za muda huu wana jukwaa,nianze kwa kuwatakia kheri ya sikukuu ya x-mass.
Ningependa kujua zaidi kuhusu nchi ya hungary,maisha yao,miji mizuri kuishi,chakula,culture,nk nk
Karibuni sana kwa michango yenu!
 
Hungary ni moja ya nchi zilizopo katikati kabisa ya bara la Ulaya.

Inapakana na Serbia kusini na kaskazini Slovakia.

Watu wa Hungary wanazungumza lugha ya Hungary Hungarian.

Mji mkuu na maarufu waitwa Budapest lakini ipo miji mingine kama Debrecen na Szeged.

Ni moja ya nchi zilizokuwa zkiunda umoja wa kisoviet au USSR na mwaka 1989 ikawa nchi huru baada ya kujitenga.
Hungary ilitawaliwa na hinaya ya Ottoman kwenye karne ya 18 na ikawa inaitwa Austria -Hungary wakati wa vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia.

Hungary ilikuwa ni nchi ya kikomunist lakini ikabadili mfumo huo na kuingia mfumo wa kibepari taratibu kupitia mkataba uitwao Warsaw pact kati yake ni nchi zingine za kisovieti.

Watu wa Hungary wana utamaduni wa kucheza ngoma kwa mtindo wa kuzunguka kwa wanawake huku wakiinama na wanaume nao wakifanya hivyo mtindo uitwao Ugros.

Hungary ina ziwa kubwa katika Ulaya ya kati liitwalo Balaton na nchi hii hali yake ya hewa ni mchanganyiko wa baridi na joto kiasi.

Hungary kuna sinagogi kubwa kabisa duniani lililojengwa mwaka 1859, pia kuna bafu kubwa kuliko lolote duniani liitwalo Széchenyi Medicinal Bath lililopo Budapest.

Kwenye hili bafu ukioga basi waondoa magonjwa ya ngozi na maji yake yanasaidia ngozi kuwa nyororo na laini.

Utamaduni wa watu wa Hungary pia umelalia kwenye chakula ambapo wana supu maarufu ambayo ni ya samaki ambae kukatwakatwa vipande na kuchanganywa na pilipili nyekundu ya paprika.

Pia wanapenda maji ya thermal hivyo kutumia zaidi spa kushinda humo kwenye maji hayo.

Profesa Philemon Sarungi ni miongoni mwa wanafunzi walokwenda kusoma nchini Hungary kwa kulipiwa na serikali ya nchi hiyo kwenye miaka ya 70 na 80 hadi mwishoni kutokana na ushirikiano kati ya nchi hiyo na serikali ya Tanzania.

Kwa kifupi ni hivyo mkuu,

Hata kata tiketi ukatembelee Hungary.

Christmas njema.
 
Ngoja nami nitafute nchi ya kuishi sio kwa post hizi nianze na finland
 
ni nchi yenye Kodi kubwa sana,ukifanya kazi utaishia kukatwa Kodi kubwa,kwa mtu single ambaye Hana family Kodi yake ktk kipato ni 35% kama unalipwa million 1 utakatwa 35% ya million 1
wananchi wake wengi wameikimbia nawaona Germany hapa wakibeba box
wengine wameungana na jiran zao wa Romania kwenye ombaomba, ombaomba maarufu hapa Germany ni wa Romania
nchi ya Hungary Ina viwanda vingi Sana,na wanatumia visa ya Schengen
ni nchi ya wakatoliki,ktk wakristo ambao ni 52%, wakatoliki ni 37%
wananchi wanashtumu uongozi wa nchi hiyo kuwa una viashiria vya kiimla hii ni kutokana n'a wazir mkuu wake Viktor Orban kuwa swahiba mkubwa wa putin
mji mkuu wake ni Budapest
cc
Jon Stephano
britanicca
 
Hungary ni moja ya nchi zilizopo katikati kabisa ya bara la Ulaya.

Inapakana na Serbia kusini na kaskazini Slovakia.

Watu wa Hungary wanazungumza lugha ya Hungary Hungarian.

Mji mkuu na maarufu waitwa Budapest lakini ipo miji mingine kama Debrecen na Szeged.

Ni moja ya nchi zilizokuwa zkiunda umoja wa kisoviet au USSR na mwaka 1989 ikawa nchi huru baada ya kujitenga.
Hungary ilitawaliwa na hinaya ya Ottoman kwenye karne ya 18 na ikawa inaitwa Austria -Hungary wakati wa vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia.

Hungary ilikuwa ni nchi ya kikomunist lakini ikabadili mfumo huo na kuingia mfumo wa kibepari taratibu kupitia mkataba uitwao Warswa pact kati yake ni nchi zingine za kisovieti.

Wa wa Hungary wana utamaduni wa kucheza ngoma kwa mtindo wa kuzunguka kwa wanawake huku wakiinama na wanaume nao wakifanya hivyo mtindo uitwao Ugros.

Hungary ina ziwa kubwa katika Ulaya ya kati liitwalo Balaton na nchi hii hali yake ya hewa ni mchanganyiko wa baridi na joto kiasi.

Hungary kuna sinagogi kubwa kabisa duniani lililojengwa mwaka 1859, pia kuna bafu kubwa kuliko lolote duniani liitwalo Széchenyi Medicinal Bath lililopo Budapest.

Kwenye hili bafu ukioga basi waondoa magonjwa ya ngozi na maji yake yanasaidia ngozi kuwa nyororo na laini.

Utamaduni wa watu wa Hungary pia umelalia kwenye chakula ambapo wana supu maarufu ambayo ni ya samaki ambae kukatwakatwa vipande na kuchanganywa na pilipili nyekundu ya paprika.

Pia wanapenda maji ya thermal hivyo kutumia zaidi spa kushinda humo kwenye maji hayo.

Profesa Philemon Sarungi ni miongoni mwa wanafunzi walokwenda kusoma nchini Hungary kwa kulipiwa na serikali ya nchi hiyo kwenye miaka ya 70 na 80 hadi mwishoni kutokana na ushirikiano kati ya nchi hiyo na serikali ya Tanzania.

Kwa kifupi ni hivyo mkuu,

Hata kata tiketi ukatembelee Hungary.

Christmas njema.
Mkuu Hungary haijawahi kua sehemu ya Jamhuri za Kisoviet. Maelezo mengine upo sahihi mkuu wangu
 
Soma kwa uzuri historia utaelewa.

Hungary wakati wa vita kuu ya pili ya dunia ilijiunga na umoja uloitwa Axis Powers ulounda nchi za Germany, Italy na Japan.

Benito Mussolini ndo alikuwa kinara wa kuunda umoja huu na Adolf Hitler akauunga mkono na wakafanikiwa kujiopolea baadhi ya maeneo ya kumiliki barani Ulaya, Afrika kaskazini na Asia mashariki.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia mwaka 1918 kulitokea mapinduzi nchini Hungary baada ya kumeguka kwa ilokuwa Austria -Hungary, na hapo ikaundwa jamhuri ya kidemokrasia ya Hungary na ikawa na waziri mkuu wake.

Hapohapo Hungary ikatangazwa kuwa ni nchi huru, lakini mwaka 1919 kukatokea mapinduzi mengine ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa jamhuri ya kisoviet ya Hungary.

Hivyo kutokea mwaka 1949 hadi 1989 Hungary ilikuwa ikiitwa satellite state ya kisovieti yaani ikifuata sera za USSR.

Satelite State maana yake ni kwamba nchi inakuwa iko huru lakini inakuwa hoi kiuchumi hivyo kufuata mlengo fulani ambapo Hungary ilijikuta ikifuata sera za kijamaa za ilokuwa USSR na hata kijeshi ilikuwa ikiifuata USSR.

Kwenye vita kuu ya pili ya dunia Hungary iliingia chini ya mwamvuli wa Axis Powers na kuanza kuishambulia USSR hiyo ikiwa ni baada ya sehemu fulani kudunguliwa na ndege za kivita zisizojulikana.

Hivyo vita ikapigwa kwelikweli kati ya Hungary na USSR upande wa mashariki mwa Hungary lakini Hungary ikagundua inapoteza wanajeshi wake kwa siri wakazungumza na nchi za magharibu kuomba msaada.

Hiyo ilikuwa ni baada ya Hungary kukung'utwa vibaya kwenye eneo la mto Don lakini Germany ikaingia Hungary na kuitawala kupitia kiongozi kibaraka Szlas na chama chake cha kifashisti.

Hungary ilishiriki mauaji ya halaiki kwa wayahudi kwa kuwaamuru wayahudi wote waondoke nchini humo na kuwapeleka Auschwitz na wayahudi zaidi ya 400,000 waliuawa.

Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 1944 Hungary ilijikuta ikiangukia mikononi mwa USSR.

Kheri ya Christmas.

Yesu amezaliwa.
 
ni nchi yenye Kodi kubwa sana,ukifanya kazi utaishia kukatwa Kodi kubwa,kwa mtu single ambaye Hana family Kodi yake ktk kipato ni 35% kama unalipwa million 1 utakatwa 35% ya million 1
wananchi wake wengi wameikimbia nawaona Germany hapa wakibeba box
wengine wameungana na jiran zao wa Romania kwenye ombaomba, ombaomba maarufu hapa Germany ni wa Romania
nchi ya Hungary Ina viwanda vingi Sana,na wanatumia visa ya Schengen
ni nchi ya wakatoliki,ktk wakristo ambao ni 52%, wakatoliki ni 37%
wananchi wanashtumu uongozi wa nchi hiyo kuwa una viashiria vya kiimla hii ni kutokana n'a wazir mkuu wake Viktor Orban kuwa swahiba mkubwa wa putin
mji mkuu wake ni Budapest
cc
Jon Stephano
britanicca

Hungary inategemea sana biashara ya kimataifa na inapeleka bidhaa nyingi sana nje.

Uchumi wake unahodhiwa na watu binafsi.
 
Back
Top Bottom