Naomba kufahamu hili kuhusu Rejesho la NSSF

Panctuality

JF-Expert Member
Jun 11, 2019
726
1,044
Habarini wadau, nizame moja kwa moja kwenye lengo la uzi.

Kumekuwa na Changio la NSSF la kisheria kwa wafanyakazi wa umma na binafsi na baadhi yenu mmekuwa mkisaidia taasisi zenu kukusanya na kudeposit kwenye control number husika.

Cha kushangaza kama inavyosemekana ni kwamba imekuwa ngumu sana fedha kuwarejeshea wahusika pindi wakomapo ajira iwe kwa kigezo cha umri au matakwa ya waajiri.

Najua mchango huu ni kwa nia njema kwamba nje na ajira kuna maisha pia hivyo fedha hizo huwa msaada.

Naomba kujua toka kwa wahusika ama wenye uzoefu na hili je, ni kweli fedha hizi huwa ngumu sana kuwarejea wahusika, na kwa kiwango gani na kwa nini wao wanaficha ukweli na kudai kuwa fedha hizi hurejeshwa kwa asilimia mia, na je hurejeshwa kwa kigezo cha umri au hata ajira ikomapo tu?

Na huchukua muda gani msaada ndugu wana JF.
 
Mkuu suala la kupata michango kwa sasa limekuwa gumu sana. Mifuko ya jamii iko kwenye kipindi kigumu sana. Ukweli ni kwamba kama una profession wanakupa asilimia mia ya full salary ya mwezi mmoja kwa mikupuo mitatu.

Yaani mfano mshahara wako ni milioni moja utapewa 330,000/= mwezi wa kwanza, wapili na watatu. Kwa hiyo utapewa jumla ya milioni 1 iliyogawanywa mara tatu.

Baada ya hapo hutapewa tena pesa yoyote hadi ufikishe miaka 55. Labda itokee una ulemavu wa kudumu unaokuzuia kufanya kazi ndio utaweza kupatiwa mafao kwa mujibu wa taratibu za mafao.
 
Pesa unaweza kupata, ila hakikisha una aidha termination letter au mwisho wa mkataba.
Mwenye Elimu kuanzia Diploma anasubirishwa mafao hata kama mkataba umeisha au ana termination letter ikiaminika kuwa atapata kazi sehemu nyingine na mchango utaendelea

Ni sauti kutoka kwa afisa mmoja wa NSSF akinieleza kwa njia ya simu nilipojaribu kumhoji.
Imekaaje hii mkuu
 
Huo ndiyo ukweli! Utaambulia mshahara mmoja wa kukustiri wakati unatafuta kazi.
 
Mkuu suala la kupata michango kwa sasa limekuwa gumu sana. Mifuko ya jamii iko kwenye kipindi kigumu sana. Ukweli ni kwamba kama una profession wanakupa asilimia mia ya full salary ya mwezi mmoja kwa mikupuo mitatu.

Yaani mfano mshahara wako ni milioni moja utapewa 330,000/= mwezi wa kwanza, wapili na watatu. Kwa hiyo utapewa jumla ya milioni 1 iliyogawanywa mara tatu.

Baada ya hapo hutapewa tena pesa yoyote hadi ufikishe miaka 55. Labda itokee una ulemavu wa kudumu unaokuzuia kufanya kazi ndio utaweza kupatiwa mafao kwa mujibu wa taratibu za mafao.
Duuuh hii ni hatari sana, u- profession wa ngazi ipi, Doctarate, Masters, Bachelor, Diploma au certificate? Maana hata mwenye certificate ya Nursing nae Ni professional kwa tahasusi yake
 
Mwenye Elimu kuanzia Diploma anasubirishwa mafao hata kama mkataba umeisha au ana termination letter ikiaminika kuwa atapata kazi sehemu nyingine na mchango utaendelea

Ni sauti kutoka kwa afisa mmoja wa NSSF akinieleza kwa njia ya simu nilipojaribu kumhoji.
Imekaaje hii mkuu
In short ili iwe rahisi kupata inatakiwa kwanza kazi uliyokuwa unafanya ilipaswa kuwa siyo ya kitaaluma, halafu unapaswa kuwa na termination letter au end of contract.

Tofautinna hapo utapewa fao la kutokuwa na ajira
 
Duuuh hii Ni hatari sana,u- profession wa ngazi ipi,Doctarate, Masters, Bachelor, Diploma au certificate? Maana hata mwenye certificate ya Nursing nae Ni professional kwa tahasusi yake
Profession means skilled personnel watakuja kuongeza nyama wengine ila mwalimu, daktari, nesi wote ni professionals. Kuna ukakasi kidogo kwenye hilo suala.
 
Pesa huchukui kwa 100% unapewa asilimia 33 nyingine utachukua kidogo kidogo
 
Hapo umepotosha wafanyakazi wa umma hawachangiwi na nssf
Asilimia 10 muajiri na asilimia 10 muajiriwa hivyo basi muajiri pia anahusika kumchangia Mfanyakazi,huenda uko sawa nina uzoefu na Amcos japo sijajua wao wako upande gani,japo kila kitu kinafanyika na kuripoti kwa serikali hiyo hiyo
 
Pesa unaweza kupata, ila hakikisha una aidha termination letter au mwisho wa mkataba.
Termination letter unaweza ukawa nayo lkn nenda rudi za kutosha mwisho unaambiwa kwa proffesionals pesa hairudishwi mpka umri ufike sababu wewe laxima utaendelea na kazi kwa kua huku umetoka kwa either mkataba kuisha au kupunguzwa
 
Asilimia 10 muajiri na asilimia 10 muajiriwa hivyo basi muajiri pia anahusika kumchangia Mfanyakazi,huenda uko sawa nina uzoefu na Amcos japo sijajua wao wako upande gani,japo kila kitu kinafanyika na kuripoti kwa serikali hiyo hiyo
Taasisi za umma zote unachangia psssf na binafsi NSSF

NB kama upo taasisi ya umma na michango yako inapitia psssf then unaweza kuaamua pia kuchangia NSSF kwa hiari inaruhusiwa pia ukawa unaingiziwa nssf na psssf kwa wakati mmoja
 
Taasisi za umma zote unachangia psssf na binafsi nssf,

NB kama upo taasisi ya umma na michango yako inapitia psssf then unaweza kuaamua pia kuchangia NSSF kwa hiari inaruhusiwa pia ukawa unaingiziwa nssf na psssf kwa wakati mmoja
Shukrani kwa kunipa ufahamu
 
Ukiwa na taaluma utapewa 33% Kwa miezi 6,Yani ukishatoka kwenye ajira unakaa Mwezi mmoja tu then kafungue FAO la kujitoa.
Barua ya termination or end of your contract ni muhimu Sana Tena sana.!
Andaa passport sizes,andaa na bank statement ya miezi mitatu nyuma.
Kwenye bank statement utafuata uko bank na isiwe na -ve balance maana banks zinakataa kukuprintia ikiwa na -ve balance.
Baada ya hapo utalipwa Kwa miezi 6 hzo asilimia 33 then Kama bado utakuwa hauna ajira unatakiwa usubiri Kwa miezi 18 Yani mwaka mmoja na miezi 6 ukimaliza hapo ndio unaenda kufungua Tena kuomba kujitoa Hapo utalipwa Pesa yako yote.
 
Back
Top Bottom