Naomba kufahamu hili Juu ya " Traffic Camera "(Tochi)

Kweli ipo kwanza maeneo ya muleba tu bukoba na ushuhuda ipo iko advance ata kuliko za kenya juu iko na kumbukumbu
Hiyo kitu ni nzuri sana mkuu!

Nikiwa natoka Arusha to Dsm naweka bundle la Halotel tuu...

Gari inatembea hadi inakaa !

Precautions::::

Mtu ukipata ajali kisa overspeed (baaada ya ku-install speedometer Gps) tusilaumiane...

Hapa nanawa mikono kama pilato!
 
inawezekana hapo kulikuwa na polisi wanaojificha wale wakawapiga picha kimya kimya
 
Asante kwa taarifa, ngoja niwe makini na mie.
 
Kuna App iko playstore ina detect camera "Tochi " ya polisi...

Ukiwa una-drive ;

1.simu yako iwe fully charged..
2. Simu iwe na bundle muda wote...
3.Washa Gps ya simu yako.
4. Fungua ile application..

-Itakuwa inakuonyesha speed ya gari yako..
- then kuna display ingine Itakuwa inaonyesha Road map , mahali ulipo na mahali Tochi ilipo ( penye Tochi pataonyesha red)

App anaitwa Speedometer Gps

Install speedometers GPS to drive over 100km/hr anytime.
ahsante sana
 
Mandella siku hizi hawa wazee wa feva trick zao ziko kama mbili kubwa za kujificha ndani ya magari private pembeni ya barabara....hasa saloon cars au noah....ukiona mahali pana hicho kibao cha kuelekeza speed ndogo...wewe angalia gari pembeni utakuta kuna moja ime park mkao mzuri wa kupiga picha mahali unapotoka wewe.....ya pili ni mtu aliyevalia kiraia amesimama barabarani mikono ameficha nyuma....ukimuangalia vzr utaona ameficha camera au toch ....so akiipenda tuu yako basi unaye.....usipokuwa muangalifu utalipa faini njia nzima....
Mind you hizi tochi za hawa jamaa zinaweza kupiga picha na kupima hio speed kabla na baada ya kuwapita hao askari.
 
Hao traffic police wapo very curious katika kuangaika na dunia, utakuta polisi kajificha hadi pua haionekani na tochi, Serikali inabidi muwatafutie CAMOUFLAGED WEAR manake hizo nguo nyeupe wengine tuna macho makali kama Mimi huwa naziona km100 kabla.
Mkuu unatumia miwani au macho ya kawaida, maana mimi ni mhanga wa hao jamaa, in fact huwa sijisikii vizuri nikiendesha si zaidi ya 50km/hr.
 
Hizo kamera mbona mie juzi nimepiga 80 na sijakamatwa tena nilifanya kusudi ili nione kama wanaona mbali, pale IMTU
Mkuu unaongelea IMTU ya tangi bovu ama? Kama ni hapo tangbovu usihofu maana trafic wa hapo na Dar nzima wapo busy na foleni au daladala, ila kama unahitaji kuona kama hizo camera zipo basi andaa cash ya kutosha halafu piga moto wa kutosha kutoka Dar hadi Wami Dakawa na kurudi, utanipa majibu.
 
Hao traffic police wapo very curious katika kuangaika na dunia, utakuta polisi kajificha hadi pua haionekani na tochi, Serikali inabidi muwatafutie CAMOUFLAGED WEAR manake hizo nguo nyeupe wengine tuna macho makali kama Mimi huwa naziona km100 kabla.
Una jicho la bundi wewe sio bure
 
Aiseee......mbona ishakuwa tabu sasa........
Kama ni hivyo......wacha tupige simu Japan........ili kuepuka maneno na watu.......maana hakuna namna nyingine........
Ni picha wanapiga polisi waliojificha. Sio za setelaiti. Sio za gps. Ni wanajificha na wengine wako mbele. Wakikupiga wanawaambia wa mbele wakusimamishe. 'Really time clock system' unahitaji miundo mbinu na camera za barabarani kibao. Hatujafika huko. Ngoja tumalize majipu kwanza...
 
Mkuu unaongelea IMTU ya tangi bovu ama? Kama ni hapo tangbovu usihofu maana trafic wa hapo na Dar nzima wapo busy na foleni au daladala, ila kama unahitaji kuona kama hizo camera zipo basi andaa cash ya kutosha halafu piga moto wa kutosha kutoka Dar hadi Wami Dakawa na kurudi, utanipa majibu.
Mkuu hata hawa wa IMTU wanapiga Tochi Kama kawa Yaani.
 
Basi walikuwa busy na daladala - maana kukamata gari ndogo ndogo Dar ni risk sana kwa hawa traffic polisi, waoga hawafahamu wamemkamata nani
 
Hakuna technologia kuubwa kiivo wanachokifanya hao jamaa ni askar mwenye tochi anakua kavaa kiraia anajificha kichakani then traffic mwenye uniform anakua mbele kama km 5 hivi kwahyo kinachofanyika ni kupigiana simu na yule traffic anataja namba ya gari na picha inatumwa kwa njia ya watsap....ndo maana wenye mabas siku hizi wanajua vichaka vya hao jamaa wanakojificha we ukiwa na haraka uliza jwa wenye mabas watakuelekeza tu.
 
Jana nilikia njiani Kutokea Singida .. Mbele ya Magugu kidogo kukawa kuna Kibao cha 50km/h Limit speed .
Kwa bahati mbaya kulikua na mazungumzo kwnye gari kitu ambacho kilinifanya nipite pale na speed ya 80 ..nimekuja kushtuka kua nilikua kwnye 50km/hr Zone baada ya kuona kile kibao kinachoashiria sasa umemaliza eneo la 50km/hr.

Tukacheka tukasema bahati yetu Hakuna TOCHI .

Tukatembea Umbali kama wa 2Km hivi . .. tukasimamishwa ... tukaambia Kuna Satelati Camera zimewapiga Picha Mahala Flani Mmepitiliza speed .

Duh kwanza nikacheka ...huku nikingoja ushahidi .,

Ushahidi wa kwanza ana namba ya gari yangu kwnye List yake ..nikasema kaandika sasa hivi au ?

Ushahidi wa pili akasema ,kaa dakika 10 ,tunangoja picha yako inatumwa (hapo ndipo nilichoka ) .. mm kwa vile nilikua na haraka sikuona haja ya kungoja mda wote huo ...nikalipa fine off nikaondoka coz kweli pale nilipitiliza ..

Mkuu eneo la Minjingu hadi babati ni hatari tupu. Ukitoka tu Makuyuni, mbele kidogo kunakuwa na askari amejificha kichakani, na ukikaribia magugu ivoivo. Hapa hata mabasi yawe na speed gani kipande hiki hupunguza kabisa. Ni kipande cha KM kama 88 hivi yaani Babati-Magugu. Sisi mara tatu yametukuta kipande hicho na faini kama kawa. Tulileta ubishi ila mwisho wa siku picha zinaongea.

Je ni kweli kuna technology ya namna hiyo Tanzania hii kunasa picha pale unapooverspeed ,au niliingizwa mjini kwa kelele za Tarumbeta .
 
Ha! Ha! Ha! Hawa watu kula yao inapatikana kwa shida sana.
 
Hivi kama barabara iko tupu (assume eneo la shule) lina speed limit ya 50km/h yaani hakuna risk yoyote ya kuleta damage kwa watumiaji wengine wa barabara halafu nikapita na 100km/h then nikapigwa TORCH ya over speed , je Speed limit is justifiable?
 
Hao askari Wanavakaa kiraia wanajificha kando mwa barabara kwakuwa wakioneka madereva wanapeana ishara za kupunguza mwenzo. Hivyo hizo bado ni speed cameras ambazo zipo more advanced hata kuchukua picha. . Heshimu alama zilizowekwa utasafiri mswano kabisa bila usumbufu wowote
 
Back
Top Bottom