Naomba kufahamishwa utaratibu wa kupata leseni ya salon(kinyozi)

kingsaula

Senior Member
Nov 19, 2016
195
139
Wakuu kama kilivyo kichwa cha habari nimefungua salon ya kiume hapa DSM maeneo ya DUCE sasa TRA kila wakipita inabidi tufunge, kwa anayejua hivi salon inaweza kuwa sh ngapi kwa mwaka?

Mimi naingiza 25 kwa siku, na utaratibu ukoje wa kupata leseni, msaada wakuu
 
Nenda Tra wape details za b'ness yako kisha watafanya makadirio, usiogope.
 
Wakuu kama kilivyo kichwa cha habari nimefungua salon ya kiume hapa DSM maeneo ya DUCE sasa TRA kila wakipita inabidi tufunge, kwa anayejua hivi salon inaweza kuwa sh ngapi kwa mwaka?

Mimi naingiza 25 kwa siku, na utaratibu ukoje wa kupata leseni, msaada wakuu
nenda tu kajieleze mkuu hasa watahitaji kujua kodi ya frem na kuingiza kwako kwa siku ili wafanye makadirio
 
Kwanza kabisa anzia TRA ili upate Tin Number,then nenda manispaa ya temeke upate leseni ya biashara yako uwe na amani
 
Iko hivi... Unachotakiwa kufanya ni kuwa na TIN number kama huna utaenda kuwaambia watakupa process za kupewa TIN na kama unayo mfano kama una leseni ya gari, ina TIN namba so utatakiwa tuu kuibadilisha iwe ya biashara.. Alafu tunapewa form ya kujaza kama ni biashara mpya.. Pamoja na hiyo form utatakiwa kuambatanisha mkataba wako wa frem/pango, barua toka serikali ya mtaa, picha ndogo/passport size na hiyo TIN namba uliyopewa.. Ukishajaza ile from na kuambatanisha vyote unapelekwa TRA kwa mtu au afisa was kukukadiria kodi yako ya kulipa ya mwaka mzima pamoja na kodi ya zuio/withholding tax ambayo ni 10% ya kodi ya pango lako kwa mwezi x12miezi jumlisha na stamp 18000 fixed. Ukishakadiriwa kodi itagawanywa mara 4 kwa mwaka ambayo utailipa kwa awamu 4 ndani ya mwaka mzima. Kisha utapewa demand note ya kwenda kulipia hizo pesa benk, kisha unawapelekea riceipt ya benk, watakupa Tax clearence certificate utakwenda nayo manispaa pamoja na mkataba wako wa pango kwa ajili ya kupawa leseni. Na huko ni hela pia sijajua leseni ya saloon ni kiasi gani lakini ina range kwenye 80, 000 mpk 150. 000
 
Mfano:kodi ya frem 150, 000 kwa mwezi, kodi ya zuio ni 150, 000*10% utapata 15000 kwa mwezi. Unatakiwa ulipe ya mwaka mzima kwa hiyo 15000*12=180, 000 jumlisha stamp 18000/= so utatakiwa kulipia 198, 000/= kisha anakukadiria kodi yako sasa utakayotakiwa kuilipa kutokana na maelezo uliyompa kuhusu biashara yako, mfano una mtaji kiasi gani pamoja na hiyo kodi uliyolipa kwa muda gani ili aangaliye mtaji wako kisha akukadirie. Mfano ktk from kuna kipengele cha mtaji uliowekeza na mapato utakayoingiza kwa mwaka.. Hapo ndiyo sehemu anayotumia kukuchinjia... Mfano anaweza akakukadiria kodi ya mwaka 300, 000 kwa kuanzia atagawanya mara 4 =75000/= ambayo utatakiwa uilipe kila baada ya miezi mi3... Hivyo kwa kuanza ili upate leseni unatakiwa uwe na 75000+198, 000=273, 000/=jumlisha mhuri was mwanasheria 20, 000=293, 000/= hii ni mbali na leseni.. Hii ni TRA tuu... Bado manispaa
Soo TRA 293, 000 +LESEN MANISPAA 80, 000=373, 000/=
 
nimekuelewa vizuri mkuu, ngja nilifanyie kazi maana wanazingua kishenzi
 
Back
Top Bottom