Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 127,927
- 244,505
Kiukweli mimi binafsi mpaka sasa sizijui wala sizifahamu kabisa faida ambazo sisi waafrika tunazipata kutoka na umoja huu wa nchi za kiafrika.
Kama wanachama wake wanasigina katiba za nchi zao waziwazi mchana kweupe , ushindi wa Maalim seif ; ushindi wa Dr Besigye kunyang'anywa mbele ya macho ya AU , kuuawa maelfu ya raia wa Burundi kutokana na king'ang'anizi Nkurunzinza , ni ushahidi wa ubutu wa AU na kwamba umoja huu hauna msaada wowote kwa waafrika .
Yapo madhira mengi sana yanayoikumba africa huku umoja huu ukitumbua macho .
Napendekeza nchi yangu niliyozaliwa ndani yake inayoitwa Tanzania ijitoe kwenye umoja huu mufilisi usio na maono wala mipango yoyote kwa manufaa ya raia wake na afrika kwa ujumla .