safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,183
- 15,867
hayo maneno yaponwazi kwamba ambaye hajaelewa tafsiri ya hadithi,kwa maana wapo wengine wataelewa mbona maneno yako wazi ?ومن لم يعرف تفسير الحديث ويبلغه عقله، فقد كفي ذلك وأحكم له، فعليه الإيمان به والتسليم له.
"...na yeyote ambaye hajaijua tafsiri ya hadithi na imefikia ukomo akili yake, basi hakuna shaka ameshatoshelezewa hilo na ameshahukumiliwa, basi ni juu yake kuamini hadithi hiyo na kujisalimisha kwake....."
usuulu ssunnah ya al imaam ahmad
Wewe kama hauelewi tafsiri ya hadithi fulani hautakiwi kulazimisha wenzio nao ati wawe hawajaelewa kama wewe,hiyo haipo,wapo watu wana ufahamu wa mbali.
Mfano nakupa : kuna mwanachuoni alipoulizwa maana ya hadithi "dunia ni jela ya muumini na pepo ya kafiri"
yule mwanachuoni akajibu "dunia ni jela ya muumini ukilinganisha na peponi kulivyo,na ni pepo ya kafiri ukilinganisha na motoni kulivyo.
hapo ndio utajionea kwamba okaay kumbe kuna ambao hawakuelewa hiyo hadithi mpaka wakamuuliza huyo mwanachuoni na akawajibu.
hivyo Hakuna sehemu pameandikwa kwamba hatutakiwi kuzielewa hadithi kwa akili zetu,huo ni ufahamu wako ndugu yangu.
Wanaopinga wanapinga ufahamu wenu na sio maandiko,ebu elewa hii hoja kwanza kwamba WALE MNAOWASHUTUMU KUPINGA DALILI UHALISIA NI KWAMBA WANAPINGA UFAHAMU WENU,ILA NYINYI MNAWABAMBIKIA KWAMBA WANAPINGA DAILI NA HIYO NI DHULMA KWA NDUGU ZENU.au andiko husika liko kadha wewe ukasema hapana sio hivyo kwasababu hii haiingii akilini,
Hii ni mifano yako iliyotoka kwako ili uipe nguvu hoja yako na wala haijatoka kwa hao unaowasema kwamba wanapinga dalili.yaani mto nile chanzo si kipo hapo ziwa nyanza? mbinguni tena? hili hapana.
Uadilifu ni kuweka mifano ambayo kwa hakika ni ya uhalisia kutoka kwa watu unaowapa tuhuma hizo na sio vinginevyo.
HAidhi hii haipingi hadithi zingine kama ile isemayo "mwenye iuburuza nguo kwa kiburi.."hadithi ya jaabir ibn sulaym Allah amridhie, kwamba mtume swala na salaam ziwe juu yake amesema: "jiepushe na kurefusha nguo chini ya kongo mbili, kwasababu kufanya hivyo ni katika kiburi, na hakika Allah hapendi kiburi."hadithi
Hivyo zipo hadithi kadhaa ambazo zinaashiria kiburi mpaka sahaba mmoja alipomuambia mtume kwamba yeye kikoi chake kinaburuza mtume akamuambia kwamba "WEWE HAUFANYI KWA KIBURI".
Kwa maana kiburi na majivuno ndio kunasababisha uharamu wa jambo hilo.
Unapotoa hadithi nyingine bado haujaivunja hadithi nyingine kwa sbaabu zote zipo katika vitabu vya hadithi.
Hivyo basi suala hili linabaki kuwa pana kinyume na mnavyolilazimisha ndugu zetu nyie wa kisalafi kwamba iwe haramu wakati hadithi zimekuja kwa lafdhi tofauti.