Jamani wanaJF. Sijawahi kufika kisiwa cha Mafia wala hata kusikia mtu akielezea kuwa ametoka ama anaishi huko. Lakini sasa nalazimika kwenda huko kwa utalii wa wiki moja, tarehe11 mpaka 17 mwezi huu. Tatizo langu ni kwamba sijui usafiri wa kwenda huko unapatikana wapi? Kuna usafiri wa aina ngapi? Upi ni salama na haraka zaidi? Gharama ziko vipi? Wapi pazuri kwa kufikia na kupata malazi na chakula safi? Tafadhali naomba maelekezo kwa mwenye uenyeji wa huko.