Najua unampenda sana yule kijana, na yeye pia kwa mwonekano anaonekana anakupenda kweli ila nakuomba umalize kwanza shule ndipo uamue kuolewa.
Maisha kipindi cha uchumba huwa sio maisha halisi kwa asilimia zote. Ni vizuri ukamchunguza vizuri ndipo uamue kumpa nafasi ya kukuoa.
Ukiona ana tabia fulani hvi zinazokukera na kukunyima amani ya moyo na kwamba huwezi zivumilia ni vizuri ukaachana nae. Kuishi na mwanaume sio majaribio. Na ndoa huwa haibadilishi tabia hata kidogo. Usidanganyike!!!!
Kama bado hujamaliza kusoma, soma kwanza, hitimu na ikiwezekana pata na ajira au shughuli ya kufanya kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Usihairishe masomo ili uolewe. Ukifanya hivyo, uwezekano wa kurudi shule ni mdogo mno. Soma kwanza na jitengenezee misingi ya kiuchumi kabla ya kuolewa hii itakuweka huru siku zote.
Usiolewe kwa sababu umebeba mimba.
Dada yangu amerudi nyumbani juzi. Tofauti na alivyoondoka, amerudi akiwa na watoto wanne. Mmewe kamkimbia kaenda kuoa mwanamke mwingine.
Chanzo cha kukimbiwa ni yeye kuzaa watoto wote wa kike. Mumewe anahitaji mtoto wa kiume.
Tumempokea kwa furaha kwani ametuletea zawadi ya nieces wanne. Huwezo nyumbani kwetu sio mkubwa sana kivile kuweza kukidhi mahitaji ya wanafamilia wote.
Huyu dada yangu alibahatika kusoma hadi kidato cha nne. Japokuwa hakufaulu kwenda advance, ufaulu wake ulimruhusu kwenda chuo cha kati. Selection zilipotoka alichaguliwa kwenda nursing chuo cha serikali.
Wazazi walijipanga kwa upande wa ada, ili binti yao aweze kwenda chuo.
Ilipokuwa imebaki miezi kadhaa ili aende chuo, dada yangu alipigwa mimba na huyu X-shemeji. Kutokana na mimba, dada yangu alijihisi kapoteza thamani yake tena kama binti, hivyo aliamua kuolewa na huyo mpiga mimba wake na kuacha kwenda chuo.
Mmewe alimuahidi kuwa atamsomesha pale mtoto wao atakapokuwa lakini badae alimugeuka na kuwa anampa kichapo pale anapokuwa akimkumbusha kuhusu hiyo ahadi ya kusomeshwa.
Hebu fikiria kama huyu dada angekuwa nesi, angekuwa na mshahara wake ni nani angembabahisha?
Alichokosea ni kuchagua Mme sahihi kati ya kazi na huyo x-mmewe. Laiti kama angekuwa na ajira angelea watoto wake kwa amani bila kuongeza mzigo nyumbani kwetu.
Mabinti jishughulisheni, ila msifanye ajira zenu zikapelekea kuwadharau waume zenu.
NIMEICHUKUA SEHEMU, MIMI DADA YANGU NI SISTER.
Sent using Jamii Forums mobile app