Naomba aliye elewa anieleweshe!

Three idiot

Senior Member
Jul 14, 2016
188
154
*TAARIFA KWA UMMA*

*KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017*

*Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.*


*Namna ya Kufanya Maombi*
*Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili* *mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.*

*Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.*

Kwa maelekezo kamili na sifa za Waombaji bonyeza hii link
TAARIFA KUTOKA NACTE KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI / APRILI, 2017 | MTILAH BLOG

NB: SHARE UJUMBE HUU KUWAJULISHA NA WENGINE FURSA HII
 
Hahahahhaha nacte vile vyuo walivyoweka na kozi zenyewe daaaa kwelii wanataka kuwapiga watu pesa zao bure daaa
 
Nacte wamefungua mfumo ili kujaza nafac ambazo zilizo bakia uko mavyuoni mwaka jana ndomana wakaandika mwaka wa masomo 2016/17.baada ya deadline ya tare 6 mwez 3 kufika mfumo wataufunga then majibu ya walio apply kutoka sasa nacte ndo watafungua mfumo rasmi coz zote zikiwa zpo full ambayo ndo wataita mwaka wa masomo 2017-2018
 
Back
Top Bottom