Hongera mpenzi, Mungu awatangulie na kuwapigania kwenye ndoa yenu
1. Mtangulizeni Mungu kwenye kila jambo. Mkimshirikisha Mungu kikamilifu hatowaacha kamwe. Na hata mtakapopata jaribu kubwa namna gani, Mungu atawapa mlango wa kulitolea jaribu hilo.
(Hakuna aliyemtumaini Mungu akaaibika). Kuna situations mtapitia, pasipo Mungu hamtoweza lolote
2. Ukawe msaidizi mwema kwa mumeo. Mke ndo mbeba kusudi la mumeo, mke ndiye mbeba maono wa ndoa yenu. Hata mumeo akitetereka kuwa strong umrudishe kwenye mstari. Msupport kutimiza kusudi la maisha yake na yeye akusupport pia. Na kila mtu ajitambue na kusimama kwenye sehemu yake sahihi. Fanya kazi kwa bidii pia, mpunguzie mumeo utegemezi (msaidiane majukumu). Maana wanaume wana majukumu jamani afu maisha magumu hawakawii kupata presha jamani. Siku hizi wote mume na mke ni watafutaji
3. Ahsante, Nisamehe. Najua huwa unaaprecite kila kitu shem anachokufanyia. Basi sasa hivi ndo ukazidishe. Mshukuru kwa Kila kidogo anachokufanyia, coz kwa kidogo hicho vikubwa vitazaliwa. Ukimkosea a khaa omba tu msamaha na yeye akikukosea akaomba msamaha msamehe tu kutoka moyoni. Vinyongo ni sumu ya ndoa
4. Usiri. Kila mtu ana mapungufu yake na kuna situations ambazo sio nzuri mtazipitia. Kuanika matatizo yenu hadharani ni kumvua nguo mumeo. Naamini kifua unacho na utamstiri bwa shem..Ukiona limekukaa sana rohoni, ongea na mwenyezi Mungu. Yeye sio kwamba tu atakusikiliza, bali atakupa solution ya matatizo yako. Usifanye Vitu vya kheri afu ukamficha mumeo na Mfanye yeye akuamini na kukushirikisha Vitu vyake pia. Usiri kati ya wanandoa unaua ndoa kabisa
5. Ziba masikio. Miluzi mingi humpoteza mbwa. Kama unavyozoa takataka na kuzimwaga nje, basi na maneno maneno ya ndugu, mashoga (bakiza wachache wa muhimu) yatupe nje hivyo hivyo. Kuna watu wameziacha ndoa zao kisa tu kuendekeza maneno ya watu. Kuna watu wanaomba huko usiku na mchana muachane. Ukiletewa jambo lenye uzito, lichunguze kwanza. Sio tu unamvaa mwenzio juu juu huna hata ushahidi, utapewa na nakozi
6. Heshima, uvumilivu, Upendo, Unyenyekevu
Muheshimu mumeo. Hakuna kitu kinampa mwanaume kifua kama kuheshimiwa. Awe na hela asiwe nazo, awe na elimu au asiwenayo ukimuheshimu utamuinua tu
Mvumilie kwa mapungufu yake. Mambo yakibuma endelea kuwa naye , Mpe moyo na kumpa support. Kwenye ugonjwa wewe ndo muuguzi wake..Tunaapa "katika shida na raha", so be there for him muda wote
Mnyenyekee mumeo bana mdekeze. Mfanye ajisikie kuwa yeye ni mwanaume
Mpende upendo wa agape. Upendo usio na sababu wala msimu. Yani Mpende tu
7. Kuna hobbies zitapungua, kuna mashoga watakaopunguzwa. Ulikuwa msichana so ulikuwa free kufanya chochote bila kuwa judged na watu. Sasa hivi unakuwa mke, uwe mke anayejitambua. Mambo ya kukimbizana na marafiki sijui yaachwe. Kila weekend kwenda kujirusha wapi sijui Mmh unapotezea tu. Behave kama mke, kuwe na tofauti ya binti na mke
8. Be your husband's bestfriend. Unajua jinsi ambavyo tunawatreat marafiki. Mshirikiane, mnashea ndoto zenu matatizo, siri na matarajio yenu, mnakuwa na crazy moments pamoja. Hata kale ka muda kakuchokana kakipita kidogo, nyie mtaendelea kuenjoy as best friends
9. Lower your expectations. Unaishi na binadamu mwenzio sio malaika, atakosea, atakukwaza, kadri mnavyozidi kuishi ndo mtagundua mengi kuhusu kila mmoja wenu.. nikusameheana tu na kubebeana mizigo..
Kabla hamjaoana mtakuwa na plans kibao. Baby mwezi wa 9 tutakuwa na mtoto, December tutaanza ujenzi etc. Nyie mna mipango yenu, na Mungu ana mipango mizuri zaidi juu yenu. Kuna mambo mtafanikiwa mapema na mengine mtachelewa. Jifunze kuridhika na mumeo, usimfananishe na waume wa wenzio. Wala usitake kuishi kama ndoa nyingine zinavyoishi. Hiyo ni ndoa yenu nyie wawili, ishini nyinyi kama nyinyi
Msiyape matatizo nafasi ya kuharibu furaha yenu kabisa. Msiyape sana kipaumbele matatizo yenu, YACHEKENI, YAZOMEENI.
10. Mawasiliano. Muwe na mawasiliano active. Kuna kitu mdiscuss, kuna taarifa peaneni, kuna tatizo au mmekwazana ongeeni. Kuanza kuishi baba anaingia, mama anatoka.. you are finished. Vunjeni ukimya, zungumzeni. Kauli zako zikawe laini na njema kwa mumeo
Mwee ngoja niishie hapa, yale mambo fulani amazing ngoja makungwi waje