Naolewa wiki ijayo, nahitaji ushauri kwa wazoefu na ndoa

Naolewa wiki ijayo, nahitaji ushauri kwa wazoefu na ndoa

Nanaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
5,893
Reaction score
3,712
Habari zenu wakuu,

Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 26.Natarajia kufunga ndoa wiki ijayo Inshaallah kama mambo yataenda kama yalivyopangwa. Naomba wale wazoefu, makungwi, manyakanga, washauri waje hapa kunishauri juu ya taasisi hii adhimu ya ndoa nifundeni jamani nikafanyeje huko ili ndoa yangu iwe tamu daima.

NB; Wale mlokata tamaa na ndoa mnaweza kupita kupita kimya kimya.

The Boss FaizaFoxy Kongosho King'asti AshaDii Descartes Himidini @Aspirin nyumba kubwa farkhina just to mention few.

Ambao sijawataja msione nimewatenga, karibuni mtiririke mnishibishe busara zenu.

Salaam.
 
usihesabu makosa, kumbuka binadamu wana mapungufu sio mmeo akikukosea basi unaweka kiburiii unapunguza upendo wanandoa hogombana sana ila baada ya kuzungumza huishi kwa upendo kama mwanzo, hakikisha chumba chako kinakuwa kisafi sana na kinakuwa na mpangilio mzuri
heshima kwa mumeo ni agizo kutoka kwa mungu
 
Sikujua kumbe The Boss umewekwa kundi la naniliu...... ( naogopa hata kulitaja)


Abyway ndoa ni vile ntakavyoishi haina fomula....kikubwa kusomana na kuchukuliana....
 
Last edited by a moderator:
Be who you are and be at your best.
Fanya yale yanayompendeza Mungu.
 
Kwangu mimi usafi wa mwili muhimu
Pia umlishe mumeo vyakula vitakavyolinda afya yake na uanaume wake,sio kila siku kujifanya we mzungu sana kumpikia mumeo chips na mayai ya kizungu na kuku wa kizungu,baada ya miaka miwili mitatu unaanza kugongwa nje kisa jamaa kala sana mivitu ya kizungu sio sifa wazungu wenyewe wanataka watu weusi wakidhani hawajawa effected
Pia ukawapende wakwezo walokuletea mume,pia ukubali kujifunza kupika kama ulikuwa hujui sio unapika wali kama unapika makande,ila kubwa zaidi ni kuwa karibu na mungu kimatendo na kiroho hili ndio litabeba yoote

Natania tu
 
haha !
wenzako watoka ati !
ndoa nikumpata yule ambae mnaelewana na asiwe mhanga wa ngono !
all the bests !
 
Mpede mmeo kama alivyo pia usiishi kwa mazoea ya hali ya furaha kila mda. Jua kuna kipind mambo yatachange mtapita ktk magumu sana we vumilia mpe mwenzako moyo sababu ni majari na ni mapito. Uwakutao huko wapende wote kwanzia mdgo hadi kizee sometime kunamaudhi ila vumilia yapuuze we ongeza upendo kwao utaona wamebadilika.
 
hongera kipenzi kwa kufukia hatua hiyo nzuri sana katika maisha. cha kwanza maombi ni muhimu sana kwa Imani yako, pili Mwanaume hapigiwi kelele, Muheshimu,mpende,Jitume kama mwanamke,hakikisha unasimama katika nafasi yako kama mwanamke,maana wengi wetu huwa tukishaolewa tunajisahau sana,mpikie chakula kitamu,kuwa mbunifu, usafi muhimu sana bibi weee,mambo ya kunuka shombo,vitu ndani hovyohovyo nguo hadi sebuleni ni mwiko.Pangilia nyumba yako vizuri sana kila kitu kikae mahala pake maana nyumbani panahitajika kuwa sehemu pa kuondolea stress.otherwise all the best na ukawe mke mwema
 
Kiufupi unaanza maisha mapya jiandae kuwa mama. Jiandae kuwa multipurpose yaani kuwa capable na mult task huku unalea mtoto huku unaipenda familia yako bila kuwasahau wazazi na ndugu zako wakati huo huo bila kuwatenga ndugu wa mume.
Kuna baadhi ya vitu itakugharimu kuviacha hata kama unavipenda vipi na kuna baadhi ya vitu itakugharimu kuvifanya hata kama huvipendi.
Hobby zako zitabadilika baadhi ya marafiki watapotea automatic n.k n.k
Kila la kheri binti la muhimu utumie akili na sio nguvu la utachoka mapema. Upoo.....!!
 
Ndoa ni ya wawili wewe na mumeo.
NAWATAKIA MAISHA MEMA YA NDOA KARIBUNI KWENYE CHAMA CHETU.
 
Back
Top Bottom