Shukrani A. Ngonyani
JF-Expert Member
- Feb 23, 2014
- 1,182
- 2,015
Wote ni viongozi ila kwa mawazo yangu huru wanatofautiana ktk maeneo mengi sana. Nitaeleza kwa niliyojifunza binafsi kwao.
1. Matumizi ya lugha. Ktk hali ya kawaida unaweza kutofautisha hawa wawili. JK ni mtaalamu wa matumizi ya lugha, anajua kupanga maneno yenye mvuto, utani, kejeli na hata kutia maneno chukwu.
2. Uvumilivu wa kisiasa. Hapa JK kamzidi JP kwani Kikwete alijua sana kuwa na subra na kuleta maridhiano ktk masuala ya kisiasa. Aliruhusu watu wamseme, wamtukane(japo ni kosa kisheria), wamkejeli nk. Naye alikuwa anawavumilia kwa yote.
3. Matumizi ya vyombo vya ulinzi na usalama. JK alijua kuwa mvumilivu na pia hata pale vyombo vya ulinzi vilipovunja sheria hakukemea waziwazi. Mfano. Mauaji ya Mwangosi kule Nyololo, kushikiliwa kwa muda mrefu kwa Shehe Ponda bila kosa(kwa mujibu wa mahakama), mauaji ya Arusha, Morogoro ktk mikutano ya CHADEMA nk.
4. Uwajibikaji. Hapa JK alipwaya sana ukilinganisha na Magufuli. Mafisadi kutanua, watumishi hewa, malalamiko ya rushwa, kujuana na undugu ktk ajira, utoaji wa huduma za kijamii ulikuwa mkubwa sana. Walau kwa sasa tunaona juhudi za kutia moyo za JM kuondoa hali hiyo.
5. Uhuru wa habari na kujieleza. Hapa JK alionesha ukomavu wa kishindo. Ktk miaka yake 10 makumi ya vituo vya radio, TV na magazeti yalianzishwa. Na wakafungia Mwanahalisi. Ukiacha adhabu ndogo zilizowapata magazeti ya Mwananchi, Mtanzania nk.
Aliruhusu uwazi ktk mambo mengi, Bunge LIVE, mikutano ya kisiasa, mijadala ya kisiasa, nk. Hakika ktk hili Kikwete ni mwamba.
Kwani hata siku za mwanzo Magufuli alipokuwa anajibu maswali ya wanahabari nilihisi jambo la utofauti. Majibu ya mkato, mzaha wenye ubabe nk. vilitawala.
6. Uongozi. Hapa tena Kikwete amempiku Magufuli nionavyo. Kikwete alikuwa mtulivu ktk kufanya maamuzi. Hakurupuki, hana jazba, hana mushkeli. Ikihitaji maridhiano yuko tayari hata kukuita Ikulu mzungumze. Yule mzee alikuwa kiongozi japo si mtawala.
Kwa maoni yangu kiuongozi bora Kikwete kamzidi sana Magufuli. Japo binafsi naamini Kikwete alizungukwa na wabaya wake bila kujijua. Ila yule mzee nilimkubali sana kiuongozi japo kuna mambo alinikwaza nikaichukia CCM yake na kuamua kupindua zumla na nikampa kura mmasai wa Monduli.
Wewe unadhani nani zaidi kati yao?