NANI WALIKUWA KIVUTIO Afrcon 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NANI WALIKUWA KIVUTIO Afrcon 2012

Discussion in 'Sports' started by TONGONI, Feb 18, 2012.

 1. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ikiwa na takribani juma moja limepiti toka ZAMBIA kutangazwa mabingwa wapya wa soccer barani Afrika nadhani sio vibaya tukijikumbusha vipaji vipya vilivyojitokeza wakati wa mashindano haya,mimi binafsi nimevutiwa na wachezaji wafuatao.

  EMMANUEL MAYUKA-ZAMBIA..Anaichezea klabu ya Young boys ya swiss,kwa umri wa miaka 20 ameonyesha kiwango kikubwa na amekuwa ni mchango mkubwa kwa timu yake ya Taifa ZAMBIA kwa kupachika mabao matatu likiwamo lile la ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya GHANA.

  PIERRE EMMERICK AUBAMEYANG-GABON..Anaichezea klabu ya Saint Etiene-France,umri miaka 22..pamoja na kuwa amewahi kuiwakilisha France under 21 aliamua kuvaa rasmi jezi ya GABON katika senior international career,pamoja na kukosa penalty ambayo iliwatowa wanyeji shirika GABON nje ya mashindani lakini alikuwa na mchango mkubwa na kivutia katika mashindano haya.

  ALAIN TRAORE-BURKINA FASO-Anachezea klabu ya Auxerre-France,umri miaka 21,ni kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kutengezeza nafasi na kufunga vile vile,ameonyesha kiwango cha juu katika mashindano haya ikumbukwe alifunga goli nzuri kwa mpira wa adhabu mechi zidi ya ANGOLA.

  EMMANUEL AGYEMANG BADU-GHANA..Anachezea Udinese-Italy,umri 20,ni kiungo mlinzi ameonyesha uwezo mkubwa hasa kwa timu inapo-pokonywa mpira,inapokuwa na mpira uwezo wake wa ku-mark uko juu,na ana sifa moja nzuri ya kuwa na bidii mazoezini na katika mechi.

  MUDATHIR EL TAHIR-SUDAN-Anachezea El Hillal-Sudan-Nadhani wengi tulishangazwa na kiwango walichoonyesha SUDAN katika michuano ya mwaka huu,na MUDATHIR alikuwa na mchango mkubwa katika timu ni mshambuliaji aliye kamilika,anauwezo wa kupiga mashuti,kupiga chenga na anashabaha ya goli,alifunga mabao mawili katika michuano ya mwaka huu.

  NITAKUWA SIKUTENDA HAKI NISIPOWATAJA -KENNEDY MWEENE mlinda mlango,STOPHIRA SUNZU nafasi ya ulinzi,ISSAC CHANSA mchezaji wa kiungo,NATHAN SINKALA mchezaji wa kiungo na bila kusahau captain aliyecheza bila kuchoka CHRISTOPHER KATONGO..
  Wa JF mnawezo kutoa mchango kwa wale walio wavutia katika michuano ya mwaka 2012.
   
 2. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimemfahamu katongo miaka nane iliyo pita huyu ni mapafu ya DUMA.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Aliyekuwa kivutio ni Pele.
   
Loading...