Blue Bahari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 2,105
- 2,608
Taifa limepondeka, Taifa lina majonzi, Taifa liko katika simanzi zito.
Watanzania wengi wana majonzi, vilio kila kona, wanaomboleza kila kona. Simanzi na masikitiko vimejaa katika vifua vyao. Wapendwa wao wametoweka, hawatawaona tena asilani. Wengine hawajulikani walipo (hatujui wako hai au wamekufa). Taifa lina majonzi, Watanzania wana majonzi…………..
Ni nani wa kuliponya Taifa letu pendwa? ni nani wa kuwaponya Watanzania waliopoteza ndugu zao?
Wakati Watanzania wanaomboleza na kuhuzunika katika simanzi zito huku wakibubujikwa na machozi yaliyojaa laana, kuna Watanzania wachache mida hii wako katika makasri yao, wako katika mahekalu yao wakipongezana kwa ushindi mnono walioupata. Wanasherehekea ushindi huku wakigonga cheers kwa kutumia vikombe vya glass vilijaa damu za Watanzania waliopoteza maisha kwa sababu ya kutetea haki zao.
Washindi hao wao hawajali machungu waliyonayo Watanzania walio wengi ambao wamesononeshwa na kile ambacho kimefanywa na Watanzania wachache (washindi) ili kujihakikishia ushindi wa kishindo. Je, ushindi huo una uhalali wowote ule ilihali nchi inanuka damu kila upande? Je, furaha ya ushindi kwa wachache inazidi huzuni na simanzi iliyotawala kwa Watanzania wengi? Kuna maana yoyote ile ya kujinasibu ushindi wa kihistoria ilihari Taifa lina majonzi ya umwagaji damu?
Kulikuwa na njia za kuepusha yote hayo; kwa nini viongozi wa wakati ule, kabla ya uchaguzi, hawakuweza kuwasikiliza wadai haki? Kwa nini viongozi waliziba pamba masikioni ili kutosumbuliwa na sauti za wadai haki? Viongozi hao waliwaita wadai haki kwamba ni “wapiga kelele wasiokuwa na hoja za maana”. Viongozi hao walifikia hatua ya kuvaa miwani ya mbao ili wasione shida wanazopitia wale walioitwa “wapiga kelele”.
Tarehe 3 Novemba, 2025 wakati mteuliwa Urais akiapishwa nilimsikia akihutubia na kutamka bahadhi ya maneno ambayo kwangu mimi naona yana ukakasi kiasi flani. Alidai kwamba kilichotokea katika machafuko yaliyosababishwa na wadai haki “si utamaduni wetu, si sehemu ya maisha yetu”. Na kudai kwamba sasa ni wakati wa kuponya majeraha ya Taifa.
Maswali yangu:
1. Siyo utamaduni wetu
2. Kuliponya taifa
Hakika maswali ni mengi na pia simanzi limejaa tele katika vifua vyetu.
Niishie hapa kwa leo.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

- machafuko yaliyotokeo ndani ya nchi si utamadanuni wetu….. hapo ni sahihi. Je, figisu za uchaguzi hizo ni sehemu ya utamaduni wetu? Na wananchi wakisema sasa yatosha, majibu kutoka kwa watawala wanasema: “huo si utamaduni wetu”. Yaani kikinuka wanasema huo si utamaduni wetu; ila ghiriba na hira za uchaguzi huo ndiyo utamaduni wetu, utamaduni ulio chini ya CCM.
- Viongozi kupuuza kero na maoni ya Watanzania huo ni utamaduni wetu? ni sehemu ya maisha yetu Wananchi kupuuzwa?
2. Kuliponya taifa
- Je, ni nani wa kuliponya Taifa letu?
- Je, ni walewale ambao kwa sasa wako kujipongeza kwa ushindi wao mnono ambao sasa wanahesabika kama waovu ambao mikono yao imelowana damu za Watanzania? Wa kuliponya Taifa ndiyo hao hao wanaogonga cheers kwa kutumia glass zilizojaa damu za Watanzania ili kusherehekea ushindi wao?
- Au tunahitaji watu wengine wasiokuwa na chembe za mashaka juu ya uadilifu wao ili waliponye Taifa?
- Au Watanzania sisi wenyewe ndiyo tunahitaji kushahuriana namna bora ya kuliponya Taifa letu?