Nani wa kuiunganisha CCM sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani wa kuiunganisha CCM sasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamende, Jul 31, 2011.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Walianza kwa kunakili sera la ELIMU (kuifanya Dodoma kuwa Education Capital)
   
 2. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  jamani nimeona ni mpongeze huyu mtanzania mwenzetu kwa mara ya kwanza ameingia bunge anajitaidi sana kupigania masilahi yetu wote au mnamtazamaje? Wadau
   
 3. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hivi busanda ina mbunge?,na ilemela je?,nisaidieni
   
 4. THE PERFECT

  THE PERFECT Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona mambo kibao mpaka chadema tuseme ndio wao wafuate Mkuu bado hujatambua kama CCM inatekeleza ILABNI ya CDM ila kwa bahati mbaya hawawizi kuitekeleza wala achana na sera ya Elim
  -MZIKI wa katiba mpya? haikuwepo kwenye ilani yao.
  -mafisadi- wao wanawaita magamba
  -
  -
  -
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  If the ideas work out efficiently, and mostly important, for the sake of the nation's welfare, why should it be a problem?
   
 6. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika uamuzi mzito ambao chama hiki kimewahi kuchukua ni huu wa sasa wa kuamua kuwatosa viongozi wengine katika stahili ya msemo maarufu wa kujivua gamba. Uamuzi huu katika fikira za kawaida ulikuwa mgumu na nakubaliana na wale wanaotoa tambo kuwa tayari chama kimekusudia kutoa maamuzi magumu. Kimsingi bado chama hakijatoa maamuzi magumu bali kimefungua njia na nia ya kufanya hivyo.

  Uamuzi mugumu utafikiwa pale ambapo watuhumiwa wa ufisadi watakapopelekwa mbele ya haki, hii ndiyo safari ndefu ambayo hakuna ambaye yupo tayari kuianza hata kwa hatua moja. Ugumu wake unakuja kwa sababu moja tu nayo ni kwa sababu watuhumiwa na watuhumu wanajuana, ni waarabu wa pembe, wanajuana vilivyo kwa vilemba vya ukoka. Kila mtu anajua boriti lililopo katika jicho la mwenzake kwa hiyo hawatishani.

  Madhara ya mgogoro huu si mema kwa chama, bahati mbaya kama usafi wa matendo ndiyo alama ya mamlaka yanayoweza kutumika kutuunganisha wana ccm, turufu hii hatunayo kwa sasa. katika hali tuliyofikia tunahitaji zaidi ya uwezo wa karisima, tunahitaji alama ya usafi wa kisiasa na uadilifu unaoonekana kwa macho na katika matendo ya viongozi. Tanzania itasalimika lakini chama nina wasiwasi. Kama kauli mbiu ya kujivua gamba ikitekelezwa ipasavyo na chama kikabaki kimoja basi CCM itatawala nchi hii kwa miaka hamsini aliyosema Samwel Malecela

  Dhana hii ilipaswa kutekelezwa sambamba na uamuzi wa Bunge lakini tukasubiri mpaka leo, na isitoshe tuliwatetea kwa nguvu zote kuwa walikuwa si mafisadi na kuwa walipatwa na ajali ya kisiasa tu, sasa leo ufisadi wao unatoka wapi? je ni kwa kuwa wao si chaguo letu katika mchkato wa uraisi? mimi sijui, hoja hii ni yenu watanzania kufa hamtakufa chamoto mtakiona.

  Nawasalimu kwa jina la bwana na kuwataka mutembee na amani ya katika mwezi mtukufu wa ramadhani.
  Wasalaamu

  Mghaka the king of Litungu
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Katika Maisha ya binadamu inafahamika na kujulikana kuwa kuna kuzaliwa kuishi na hatimae kifo kwa Mwanadamu yoyote yule.Kwenye bishara na shughuri nyingine kuna Mzunguko wa biashara kisayansi ambao unaitwa LIFE CYCLE [Yaani kama Mwandamu biashara nayo inapitia Mchakato uleule wa binadamu wa kuzaliwa kuisha na hatimae kufa kwa shughuri ama biashara husika].

  Ilikufa TAA ikazaliwa TANU,Ikafa TANU NA ASP kikazaliwa Chama Cha Mapinduzi [CCM],sasa yapata miongo mitatu [3] toka kuzaliwa kwa CCM.Kwa kuwa zama [NEW ERA] hizi sasa ni mpya, zilizosimama kwenye dunia mpya yenye siasa zinazosuguana na UTANDAWAZI [Globarization] na hivyo kuifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja na kuwafanya binadamu wa zama hizi kuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo mengi haswa katika uwezo wa kuwasiliana na kupashana habari duniani.

  Hivyo CCM kwa ujio huu wa UTANDAWAZI toka miaka ya tisini inaweza kuwa na tathimini ya kuijpima uwezo wake juu ya kukabiliana na mawimbi mapya ya kizazi kipya kisicho itaji kujua na kukalilishwa kuhusu AMANI na UMOJA,bali kufundishwa jinsi ya kulinda AMANI hiyo isipotee kupitia vyama vyovyote ama kupitia taasisi yoyote ile.

  Kwa kuwa CCM inajijua na kutambua malengo ya kuanzishwa kwake,haina budi kukaa na kuona namna mpya ambayo kwa kuanzia kaurii mbiu ya kujivua gamba ni vyema wakaenda mbali mpaka kubadilisha jina na kusisi KATIBA MPYA na ITIKADI MPYA ya Chama cha Mapinduzi yenye maono [Vision] ya CCM MPYA yenye kukabidhi vijiti vya mbio kwa kizazi kipya [New Generation Dotcom].

  Kwa kuwa kutokukabidhi mbio hizo za vijiti kwa kizazi kipya na kuondoa ndani ya CCM tabia ya huyu ni mwenzetu,na CCM ya wafanya biashara na wachumia tumbo,ni hakika CCM itakuwa imejichimbia KABURI kama chama husika na pia viongozi wake watakuwa ni wahanga wa kile walichokitenda na kukiasisi wenyewe na hivyo kulipia vibaya sana.

  Sasa ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au ni heri zimwi likujualo kwa kuwa alikuli likakwisha.CCM wabadilike na kuasisi mabadiliko Wananchi wanayoyataka kwa dhati yao ya moyo.Tofauti na hayo na viongozi wapenda ubwana na utukuzwa wa kukubaliana na viongozi wajivuni na wapenda kuabudiwa kukubali kutayarisha vikwazo vya kuzuia ustawi wa demokrasia kama huo mpango unaotajwa wa kuundwa kwa sheria mpya inayohusu maandamano,wananchi watakapochua hatua dhidi ya askari mmoja kwa Wananchi elfu kumi ni risasi ngapi zitatoka kuwazuia wasiandamane.Hapa ni kuangalia Wananchi wanataka nini?Kisha kupitia CCM wananchi wapewa jibu sahihi na katika muda sahihi.Vinginevyo wakilikosa jibu hilo watalitafutia kupitia chama kingine.Na kwa dhahili hivi sasa inafahamika kuwa Wananchi wanaanza kupata imani na kutambua kuwa kumbe kupitia CHADEMA wanaweza kupata JAWABU sahihi la Matatizo yao.

  CCM BADILISHENI JINA LA CHAMA,KATIBA YA CHAMA NA ITIKADI YENU MPYA ITAMBULIKE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kama hamuamini endeleeni na jina hilo na katiba yenu na wananchi wasijue ITIKADI YENU,na hakika 2015 CCM itapasikia Magagoni kama KANU ilivyoisikia IKULU YA KENYA.

  Nasilisha
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  CCM iunganishwe ili iweje?
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  thanks kwa kwa kuwakumbusha lakini wamelala hawawezi kufanya ulicho kishauri
   
 10. n

  niweze JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kikwete na wanachama wao
   
 11. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Akifanikiwa basi atakuwa amefanya kazi kubwa sana kwa sababu karibu kila mtu Ana kundi lake ndani ya chama.
   
 12. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuunganisha ccm ni sawa na kugandisha chungwa kwa super glue.ni kitu ambacho hakiwezekani.labda wamfufue mwalimu butiama
   
 13. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  wamekwisha hawana jipya tena
   
Loading...