Nani Msafi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani Msafi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lawkeys, Feb 27, 2011.

 1. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikifuatilia threads za michango mbalimbali ya wanazuoni hapa jamvini. Nimeshuhudia watu wengi kwamba wanaitakia meme nchi yetu. Watu wanajazba kali dhidi ya ufisadi, rushwa na ubadhilifu wa mali za uma.

  Lakini bado nina wasiwasi kama kweli kuna msafi. Ni rahisi sana kuvutwa na msukumo wa kimapinduzi wa Libia na Misri, tukatamani hiki kibunga kipitie na kwetu huku. Shaka yangu juu ya Misri na Libia na sehemu nyingine dunia ambako kimbunga Karevolution kinapita, kwamba hivi watu wanasukumwa na nia ya dhati ya mabadiriko? au tu ni kama kipindi cha mkoloni kwamba, tukamwondoa lakini tulifanikiwa tu kubadilisha rangi ya mnyonyaji.

  Una hakika gani kwamba aliyeshika bango "tumechoka na ufisadi" kwamba yeye msafi. Nadhani tunapo yaona hayo tufanye mabadiliko kwanza ya nafsi. Hata kutumia muda vibaya kijiweni huo pia ni ufisadi. Tusije tukawa mafisadi kasoro nafasi. Kabla ya kufikiria ya Misri fikiri ya nyumbani kwako, mfano, unapo toka nje ya ndoa yako, unapomdhulumu mtu haki yake, huo ni ufisadi tu.

  Ufisadi, nina hakika haukui, ila nafasi ya kufanya ufisadi mkubwa ndio inaongezeka. Hivyo fisadi dagaa na fisadi papa hawana tofauti isipokuwa tu kwa kina cha maji wanapo ogelea. Most of us we are corrupt minus opportunity. Sasa, unapochangia thread za kimapinduzi usisahau mapinduzi yako binafsi.

  Tusishabikie tu! Kwamba tufanye ya Misri, hapana! Una uhakika kwamba fisadi dagaa akipelekwa kina kirefu hatakuwa Papa huyu.

  Challange kwako mwanamapinduzi. Usnikoti vibaya hapa. Ninataka mapinduzi ya kweli na mimi pia..
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ujumbe umefika mkuu!!! :rain:
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Uko sahihi. Lakini ili siyo swala la imani. Hatuwezi kungoja wote waokoke ili sote twende pamoja peponi. Kama wachache wenye mwamko wanaweza kuleta mapinduzi hakuna haja ya kuwangoja ndumila kuwili. Tutawashughulikia baada ya kuidhibiti mbingu.
   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Usijidanganye kuwa unaweza kufanya mapinduzi then ukajiuliza what is next.
   
 5. t

  tarita Senior Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hiyo?? Come out, tufanye nini?!!
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mapinduzi ya kweli ni yapi???
   
Loading...