Nani mratibu wa huu upepo?

Nani mratibu wa huu upepo?

Comi

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
3,328
Reaction score
958
Sijawahi kuona wala kusikia nchi inayoongoza kwa upepo kama tanzania, yaani na huu upepo ni kama unapangwa maana pepo zote mpya zinapeperusha kama siyo kuziondoa kabisa pepo zilizotangulia. Mf.

1. Palikuwa na hoja ya kukamatwa mafisadi.
2. Hoja ya rada.
3. Hoja ya richmond
4. Hoja ya mabomu na wananchi kuuawa na jeshi la polisi
5. ....
6. .....

Mda huu ni kuhusu madawa ya kulevya. Hivyo hakuna tukio wala hoja iliyopata ufumbuzi wala kutatuliwa imekuwa ni mambo ya kuunda tume. Je tutafika kwa mwendo huu? Nani mratibu wa haya matukio? Je tukio linalofata litahusu nini?

Viongozi waache kutoa/kutatua matatizo kisiasa,kindugu ili wananchi wapate kujua hatma ya matatizo yao
 
Ogopa sana mtu kuujua udhaifu wako, se
rikali ya ccm kwa kujua ufhaifu wa Watanzania katika kufikiri, kuchuja mambo na kuchukua hatua utumia matukio kuendesha nchi toka chaguzi moja hadi nyingine.Na hivyo ndivyo hunufaika.
 
Kwa sasa hata upepo uendeje, wananchi washajua hii tactic. Hawataki kuyumbishwa tena. Wanaujua ukweli na wanajua nani wa kumchagua. Tungoje mda ufike tuone.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sisi wenyewe tumegeuzwa upepo " huyumbishwa kila upande upepo unapo puliza " Basi tujifunze kudensi na upepo!!
 
Back
Top Bottom