nguluvisonzo
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 515
- 72
Habari za leo wana JF
Zitto ameanzisha mvutano mpya na serikali,nilisoma habari kuwa serikali inakopa kwa ajili ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wake na hata wabunge hawajalipwa,kwa upande wa waziri amesema haidaiwi na mbunge hata mmoja,sijaelewa nani mkweli.
Suala la serikali kukopa kwa ajili ya wafanyakazi wake nilikwisha wahi kusikia lakini sijui kwa kiwango gani,tena nilisikia tetesi kuwa huwa wanakopa NMB ndio maana hiyo benki huwa inatangaza faida kubwa sana.Kama ndivyo basi iko shida kubwa kwa serikali yetu na maliasili zote zilizopo leo wakope benki kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi wake,hi serikali itakuwa imepoteza mwelekeo kupita kiasi maana sasa serikali itakuwa inaendeshwa na hao wanaoipa fedha kwa ajili ya matumizi yake kwa ujumla,na je ni NMB pekee, kama nilivyosikia au kuna taasisi nyingine ? Wana JF wenye habari za kuaminika juu ya serikali kukopa naomba watupatie details,au wenye kuwenza kulifanyia uchunguzi wa kina naomba watupatie taarifa rasmi baada ya uchunguzi,ya Zitto inaweza kuwa mahala pa kuanzia.
Masikini Tanzania nchi yenye asali, lakini watanzania wanyonge hawana ndimi ndefu za kulambia matokeo yake viongozi na wageni wanalamba kwa ndimi zao ndefu na zenye nguvu mpaka wanapaliwa.