Nani kasema siasa na dini zinakinzana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani kasema siasa na dini zinakinzana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Sep 30, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Zaidi ya miaka 100 iliyopita, mwanaharakati wa siasa za mapambano, Karl Marx, alidai kwamba, “dini” ni bangi inayolevya na kupumbaza watu, wasiweze kujua adui wao wala kupigania haki zao.

  Kwa mtazamo huo, Marx aliona dini kama taasisi inayopinga mapinduzi ya wanyonge, wenye kuonewa na kunyanyaswa, akatangaza vita dhidi yake.


  Ni kwa sababu hii, mpaka leo dini [kanisa] havikai meza moja na itikadi za ki-Karl Marx, kwa maana ya Ukomunisti na dhana zingine za kimapinduzi za mwanadamu duniani.

  Kabla ya hapo, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, mwasisi wa Ukristo, Yesu Kristo [Nabii Issa], wakati akijibu mashtaka dhidi yake kwenye kesi ya uhaini, kwa tuhuma za kutaka kupindua Serikali ya Kaisari, alipewa mtego, aeleze ni kwa mamlaka yapi alielekeza utii wake; naye akajibu,“Cha Kaisari apewe Kaisari, na cha Mungu apewe Mungu”.

  Hapo ndipo ikazaliwa dhana ya kutochanganya dini na siasa, tafsiri ambayo imewasilishwa kwa kupotoshwa katika jamii mara nyingi.


  Katika makala haya nitatumia neno “kanisa” kumaanisha jumuiya za waumini wa dini mbali mbali katika jamii pana inayotawaliwa, bila ubaguzi wa ki-madhehebu.

  Kwa kifupi, kanisa ni waumini wa dini chini ya madhehebu mbali mbali, na si majengo ya kuabudia kwa madhehebu fulani fulani tu.


  Kwa Karl Marx, dini na kanisa vilikuwa ni vyombo vya watawala na wenye elimu, vilivyotumika kuwakandamiza na kuwaogofya

  [juu ya moto wa milele], kuwadhibiti na kuwapumbaza wanyonge kwa ahadi ya “ufalme wa mbingu”, kwa kujikana wenyewe ili wasielewe chanzo cha matatizo yao yenye kusababishwa na binadamu wenzao.

  Kilicho wazi hapa ni kwamba, upofu wa Karl Marx haukuwa juu ya dini, bali ugomvi wake ulikuwa juu ya watawala na mwenendo wa Kanisa kwa kutekwa na ubinafsi wa watawala, wakachanganya dini na utawala kuzaa kinachoweza kuitwa taifa na utawala wa Kiotheokrasia, kwa maana ya Taifa kuongozwa kwa misingi ya kidini, au Serikali ya makasisi.

  Wapo waliomtangulia Karl Marx ambao waligundua udhaifu huo wa Kanisa pekee la Roma la wakati huo [lililotekwa nyara na watawala tangu enzi za Mfalme Constantine wa I], lakini hawakushambulia dini, badala yake walishinikiza kufanyika marekebisho katika mfumo na mwenendo wa Kanisa bila kuathiri imani na nafasi ya dini katika jamii.

  Hawa ni pamoja na Mchungaji Martin Luther [1483 – 1534] aliyeanzisha Tawi la Kilutheri la Kanisa la Roma; Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza aliyejiengua na kutangaza Kanisa lake la Anglikana; na John Calvin [1509 – 1547] aliyebuni mapokeo ya Ki-Kalvin, kwa kutaja matukio machache tu.

  Wakati wa enzi za Karl Marx, kulikuwa na dini kuu mbili za Kimataifa yaani, Ukristo na Uislamu. Misahafu ya dini hizi ni Biblia [Ukristo] na Kurani kwa Uislamu. Kinyume na fikra za Karl Marx, misahafu yote miwili inatetea wanyonge na kupiga vita uonevu, ukandamizaji na unyonyaji, na kutoa wito kwa wanaoonewa kuasi dhidi ya vyanzo vya uovu na maovu. Kama Marx angeisoma vyema misahafu hiyo miwili bila kuyumbishwa na matendo ya watawala walioliteka Kanisa, wakaitumia dini kwa manufaa yao, bila shaka asingejenga uhasama na ukinzani kati ya falsafa yake na dini, badala yake angekuwa mtetezi mkubwa wa dini na Kanisa.

  Tuchukue mfano wa uanaharakati na uanamapinduzi wa Kristo: Kuna wakati Kristo alizua ukinzani na watawala kwa kuwataka wajisafishe kwa maovu, uonevu na dhuluma kwa wanyonge, kitendo kilichosababisha akamatwe na kusulubiwa kwa tuhuma za kuchochea maasi dhidi ya utawala wa nchi. Kati ya wanafunzi wake 12, wawili kati yao, Simon na Yuda, kabla ya kumfuata, walikuwa wanaharakati, wakereketwa [zealots] wa haki na wapiganaji dhidi ya utawala wa kikoloni wa Kirumi nchini Uyahudi.

  Uanamapinduzi wa Kristo unathibitishwa pia na maneno kama, “Nimekuja kutupa moto duniani”; au, “Sikuleta amani, bali upanga” [Luka 12: 49 – 53] kwa maana ya mapambano ya ana kwa ana dhidi ya udhalimu katika jamii.

  Na kwa sababu jamii ya wakati huo ilikuwa imejaa maovu, kama ambavyo Taifa letu linaelekea kugubikwa na rushwa kubwa na ufisadi, palitakiwa wachache kujitoa mhanga kwa manufaa ya walio wengi kama yeye alivyojitoa. Na ili kufanya hivyo alisema, “Mtu ajikane mwenyewe na anifuate”. Hata siku ya kusulubiwa kwake msalabani, hakujutia vita aliyoianzisha; akawaagiza wafuasi wake wauze kanzu [nguo] zao, ili wanunue mapanga kuendeleza harakati za kuwakomboa wanyonge.

  Kuhusu utajiri wa kinyonyaji, aliwaonya watawala wenye uchu wa kutajirika, kwamba hawawezi kutumikia mabwana wawili, Mungu [watu] na mali [utajiri] bila kuteteresha ukweli na haki; akasema, ni rahisi ngamia [kamba nene, sio mnyama] kupita kwenye tundu ya sindano, kuliko tajiri [uchu wa mali] kuuona ufalme wa mbingu, kwa njia ya kutenda haki na kweli.

  Aliwanyuka mijeledi wezi na wafanyabiashara, walioweka mbele maslahi yao binafsi kuliko utu, alipowakuta wakiuza bidhaa kwa ulanguzi hekaluni. Ikulu, kama lilivyo hekalu na msikiti ni mahali patakatifu; kwa sababu ndipo maamuzi makuu hutokea. Ni dhambi kubwa kwa wanasiasa, kama ilivyo kwa waumini kupageuza mahali patakatifu kuwa pango la walanguzi, kama alivyobaini Mwalimu Nyerere mwaka 1990, alipoona wafanyabiashara matapeli kuizoea Ikulu, Rais na familia yake.

  Usawa wa binadamu katika jamii umesisitizwa vizuri pia katika Kurani tukufu kwa kuhusishwa na zaka [zakat] na sala kuwawezesha masikini kuendesha maisha mazuri kama binadamu wengine [LXX: 24 – 25].

  Kurani tukufu inasisitiza pia juu ya utu na wajibu wa kila mtu kwa jamii [jamaa], mshikamano katika usawa, na ushirikiano kwa jamii nzima [XVII: 70].

  Uislamu, kama ulivyo Ukristo, unasisitiza HAKI, wema, usawa na ukweli kwa watu wote, hata kama hayo hayatamfurahisha muumini mwenyewe, wazazi au ndugu zake [IV: 135].

  Karl Marx hakuweza kuzitekeleza kwa vitendo nadharia zake, kwani alifia uhamishoni Uingereza kama mkimbizi na kuacha mabunda lukuki ya vitabu vya fikra zake.

  Katika zama zetu hizi, je, dini ina nafasi yoyote katika maendeleo ya jamii au bado ni yale yale ya mtazamo wa Karl Marx? Nini chanzo na sababu za watawala kutaka viongozi wa dini wasichanganye siasa na dini? Ni kipi hicho kinachoitwa kuchanganya siasa na dini?

  Ukichunguza kwa makini, utaona kuwa mambo yanayopigiwa kelele na viongozi wa dini, na ambayo watawala wanadai ni kuchanganya siasa na dini, ni pamoja na mambo kama: Tofauti
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.jpg Fashisti Adolf Hitler.jpg Karl Marx.jpg
  j.k.nyerere fashisti adolf hilter karl marx
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kuna mambo inapaswa kuyaangalia kwa umakini na ndipo tunaweza kutoa comments zenye mshiko...mfano,ni kitu gani kinacholeta kutofautiana kati ya group moja na lingine katika kila nyanja ya maisha.....maana hata hao wakristo wanatofauti zao ambazo wakati mwingine zinaleta hata uvunjifu wa amani,kupitia kurushiana maneno nk...

  Lakini pia uislamu pia una tofauti zake na mnakumbuka kwenye Idd juzi wengine walifungua mapema kuliko wengine mpaka Redio moja ya pale Morogoro(Radio Imaan) wakaingia katika mgogoro mkubwa na Bakwata...Tofauti za watu ni itikadi na sio sehemu walipo......Dini na siasa ni vitu vinavyotofautiana itikadi/unaamini nini? Ni kweli kuwa dini kwa kiasi kikubwa hata kipindi cha ukoloni karne ya 18 mpka 19 ilitumika kama silaha ya kuwagawa watu hasa waafrika kwa lengo la kuwatawala...

  Lakini kwa mtu anayeijua dini vizuri,hasa ya ukristo(natolea mfano maana ndio nayoifahamu vyema) inaimiza watu kuwa wema kati yao,umoja,mshikamano nk..hakuna sehemu katika biblia ianyosema tuwatenge wasio waamini wa ukristo...

  Sasa kipindi cha kristo aliposema ya "kaisari mpeni kaisari na ya Mungu mpeni Mungu" yatupasa kujua aliyasema haya akiwa katika mazingira gani na kwanini? swali hili lilikuwa ni mtego kwake,maana walikuwa wanataka kumfunga kwenye mtego wa kupinga serikali ya Rumi...na baada ya kujua janja yao akasema maneno hayo..kwa wale wasomi wa biblia wanajua hatua waliyochukua wale askari..kimsingi waliondoka kimya...

  Kimsingi siasa ni mapambano na wakati mwingine hata vita ikibidi,japo uwa tunaficha ukweli huu kwa kusema siasa sio mapambano,na anayesema hivyo hajui siasa maana yake ni nini... Siasa ni matumizi ya mbinu mbalimbali hata ikiwezekana mapinduzi ili mradi upate dola,kwa maana hii ndogo tu uwezi ukaweka pamoja dini na siasa hata kwa dawa...

  Ni kama maji na petroli, japo kwa upande mmoja dini inaheshimu siasa na Mtume Paulo aliwai sema wakati akiwaandikia Warumi.."Kila mtu anawajibu wa kuheshimu mamlaka iliyopo,maana imewekwa na Mungu..akaendelea kusema,maana watawala hawawatishi watendao mema bali wale waendao kinyume na mamlaka" Kwa mantiki hii naweza kusema itikadi ndio zinasababisha dini na siasa...

  Nawakilisha mkuu...........
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Nimesoma kitabu kimoja kinachoitwa VITA DHIDI YA UGAIDI kilichoandikwa na YERICKO Y. NYERERE Kuna sehemu amezungumzia "uhusiano wa siasa za dunia na dini" nitaomba ni nukuu andiko lake hapa:   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Binafsi nimeipenda falsa iliyotumika kwa hapa tz maana bila hivyo sijui ingekuwaje!
   
 6. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uislam ni mfumo pekee duniani ambao hautaji mfumo mwingine toka nje ya uislam ili utimie au ufanye kazi! ndiyo maana unasharia zake! upo wazi kiasi unafundisha jata jinsi ya kunya (oops!! Kujisaidia am sorry jamani) lakini huo ndiyo ukweli! Sasa anayejaribu kuuchanganya na hii mifumo mingine huyo atakuwa dhalili tu. OLE WAO HAO SHURA SIJUI ZA MAIMAMU, SJUI BASUTA, SIJUI, RADIO IMANI NA HAO WAKUBWA ZAO BAKWATA!! kujifanya kwao na mseto wa dini hii iliyokamilika na siasa za Tanzania.
   
 7. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sometimes dhana ya Karl Marx ina mashiko flani!
  Kikubwa ni kuwa waangalifu katika kuyashughulikia maswala hayo mawili.
   
Loading...