Nani kamuuzia Manji ufukwe wa Coco?

Nani kamuuzia Manji ufukwe wa Coco?

Miunda;
Usikitamke chama hicho tena mkuu. Wanasema atii, Magu hajachangiwa hata senti moja na mfanyi biashara. Wakati tunajua kuwa hawa ndio walio mfadhili akaingia Ikulu. Sasa unataka wafanyeje kama kurudisha fadhila?
Matokeo yake ni mkuu wa mkoa akamlilie ukiwa kuwa masela wameng'am. Hakuna uwezo wa kumgusa mteule. Sasa atakuwa meya wa jiji ndo mtalijua jiji

Haha, pole yetu
 
mkuu wa mkoa na ukali wake waoote anamuomba manji pesa balaaa, makonda kimya kabisa?
 
Watanzania wenzangu wakati umefika sasa wakusema basi Kwa baadhi ya viongozi wetu wanaojifanya wanatoa maamuzi Kwa niaba ya serikali kumbe in Kwa faida yao binafsi.Inashangaza Leo Mkuu Wa Mkoa eti anamsihi Manji aachie eneo la COCO BEACH Kwa ajili ya wananchi.Kwani ni nani aliyemwuzia Manji? Je huyo aliyeuza hakujua kuwa kuna wananchi? Ni dhahiri uongozi Wa mkoa haukuhusishwa .Kuna wakati watendaji Wa Wizara ya Ardhi waliuza eneo la Mnazi Mmoja Kwa mfanya biashara aitwae Bagdadi lakini Aliyekuwa Waziri Wa Ardhi Mh.Lowassa alizuia biashara hiyo Na wahusika wote akiwemo Na Bagdadi mwenyewe walifikishwa mahakamani Na kuhukumiwa vifungo.Wakati umefika Wa Mkuu Wa Mkoa sio kumwomba Manji ila kutengua mikataba yote Na wahusika wote wafikishwe mahakamani.Wahusika wamefanya biashara Na Manji.Kauli mbiu yetu ni HAPA KAZI TUU

Ni bahati mbaya sana watu wanasikiliza majungu ya mitaani. Mpaka waka mpotosha Rais wa nchi kuwa Manji kanunua. Ni hatari sana kwa watu wa karibu na rais kumtia maneno yasio kweli.

lini manji kanunua hio Coco beach ? Huo ukanda haujauzwa. ni hatua ya manispaa kutaka kuuendeleza kwa JV. Na kwa bahati mbaya sana hawakufanya hilo kwa uwazi ...waliingia mkataba na manji kuliendelza lile eneo kwa makubaliano maalum.
hakuna alouziwa kitu...ila watu walimlisha maneno rais nae akaingia kichwa kichwa na na bado suala linapotoshwa . mwenyewe manji amekaa kimya kwa sababu anashangaa tu ...
 
Na nani kammuzia jengo la iliyokuwa ETIENNES HOTEL pale eneo la Upanga? Jengo hilo la kihistoria lilikuwa mali ya umma kupitia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Rais Magufuli majuzi amesema kuwa kwa wenye pesa hata Ikulu inanunulika. DG Mchechu tuambie nani alitoa kibali cha kuuza na mliuza kwa bei gani?
rais@ikulu.co.tz
 
Hata hivyo, mali za uma huwa zinauzwa kwa tenda (disposal of public assets is through tendering) Mbona hatukuwahi kusikia tenda imetangazwa?
Alafu kuna wafanya biashara wengine ambao wana allergy na vitu vya halali. Yani kuna watu kila dili wanalopiga lazima linaleta lawama. Au ndio mashariti waliyopewa na mganga nini?
 
Ukweli uko hapa..huu mradi ulianza zamani na halmashauri haina pesa wa kuuendeleza....Kama hakuja manji kuwekeza atakuja Mangi au Jecha..wote Watanzania...na ingawa inasemwa hakuna kiingilio ..hilo ni siasa zaidi kwani hawa watakao endeleza eneo hili watataka kurejesha fedha yao. Investments yoyote inatazamwa ROI Ni kiasi gani kwa mwaka...
Enjoy Video Ya Coco beach Mpya kwa faida yenu. na tuache Kupiga porojo

Last edited by a moderator:
Acheni kupepesa macho manji kauziwa na tibaijuka. Bhagdad aliuziwa na lowasa. Hata uwanja wa nyamagana mwanza ulishauzwa kwa moil.
 
Miunda;
Usikitamke chama hicho tena mkuu. Wanasema atii, Magu hajachangiwa hata senti moja na mfanyi biashara. Wakati tunajua kuwa hawa ndio walio mfadhili akaingia Ikulu. Sasa unataka wafanyeje kama kurudisha fadhila?
Matokeo yake ni mkuu wa mkoa akamlilie ukiwa kuwa masela wameng'am. Hakuna uwezo wa kumgusa mteule. Sasa atakuwa meya wa jiji ndo mtalijua jiji

We mjinga sana, yaani umesha jua yote hayo
 
Watanzania wenzangu wakati umefika sasa wakusema basi Kwa baadhi ya viongozi wetu wanaojifanya wanatoa maamuzi Kwa niaba ya serikali kumbe in Kwa faida yao binafsi.Inashangaza Leo Mkuu Wa Mkoa eti anamsihi Manji aachie eneo la COCO BEACH Kwa ajili ya wananchi.Kwani ni nani aliyemwuzia Manji? Je huyo aliyeuza hakujua kuwa kuna wananchi? Ni dhahiri uongozi Wa mkoa haukuhusishwa .Kuna wakati watendaji Wa Wizara ya Ardhi waliuza eneo la Mnazi Mmoja Kwa mfanya biashara aitwae Bagdadi lakini Aliyekuwa Waziri Wa Ardhi Mh.Lowassa alizuia biashara hiyo Na wahusika wote akiwemo Na Bagdadi mwenyewe walifikishwa mahakamani Na kuhukumiwa vifungo.Wakati umefika Wa Mkuu Wa Mkoa sio kumwomba Manji ila kutengua mikataba yote Na wahusika wote wafikishwe mahakamani.Wahusika wamefanya biashara Na Manji.Kauli mbiu yetu ni HAPA KAZI TUU

Yeees! Zero tolorance to corruption! Wahalifu na mitandao yao yote hawabembelezwi bali wanastahili kutajwa hadharani, kuaibishwa na kuadhibiwa, period; vitendo na kauli za kina Anna "Mugambile" Tibaijuka vinatosha kuacha kuvumilia wahalifu wa aina zote.
 
We mjinga sana, yaani umesha jua yote hayo

Lib Socialist;
Naona huenda kiswahili kilikupiga chenga kidogo. Ati kwako mjinga anayajua mambo. Tunasemaga hivi;"We mjanja kweli, kumbe umeshayajua hayo yote?" Wajinga ndo waliwao, nasi hatukubali kuliwa tena na Manjiiiiiii. Tutapaaza sauti zetu mpaka sikio lake lisikie pamoja na utomvu wa pesa yake kuliziba. Chezea upinzani weye. Hapa ni Hakiii, sema; Sawa kwa woteeeeeee
 
Inakuwaje manispaa ya kinondoni wamuuzie,
Afu hao hao wakakate rufaa mahakamani ya manji kushinda kesi ya kuuziwa kiwanja hicho???
Kuna mawili: 1.Inaonesha kwenye mkataba huu manispaa ya kinondoni ili 'the weaker contracting party' na Manji akawa 'the stronger contracting party'.. Hivyo Manji akaweza kudictet baadhi ya vipengere vya mkataba. 2. Huenda wakati mkataba unafanyika manispaa ya kinondoni 'hawakuwa of free'... kuna nguvu iliyosukuma kwenye mkataba huo. suala ni nguvu ipi ilikuwa nyuma ya huu mkataba?
 
Back
Top Bottom