Mwl.Nyerere mnamo 1995 alizunguka nchi nzima akimnadi B.Mkapa wakati wa kampeni za urais; akisema Mkapa alikuwa mtu safi. Watanzania wakaamini kwamba Mh.Mkapa alikuwa mgombea safi.
Miaka 10 ikashuhudia Mkapa akihusishwa na kashifa kibao,ikiwemo kuuza mashirika ya umma ambayo kwa mujibu wa mwl. Nyerere hayakupaswa kuuzwa,kwani yalikuwa yanaliingizia taifa faida kubwa.mfano wayo ni pamoja na benki ya NBC. Mkapa huyo huyo,Mr. Clean, akatuhumiwa kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa shilingi milioni 70.
Ukiangalia tu,,hakika Mh.Mkapa alikuwa msafi.Aliingia madarakani akiwa msafi. Alitoka madarakani akiwa na shutuma nyingi, hata kufika mahala,watanzania wakadokezwa kwamba " ati" kifo cha mwl.Nyerere kilikuwa na mkono wa serikali yake.
Kwa muktadha huo, Mh.Magufuli yeye sio msafi.Anagombea urais akiwa na tuhuma kibao,mojawapo ni ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali inayosema Wizara ya Ujenzi chini ya Magufuli imefisidi shilingi bilioni 230.
Tukichukulia kuwa ccm ni kama mtambo wa kuwabadili wasafi kwenda kwenye wachafu.Huyu mh Magufuli ameshatuhumiwa uchafu.Uchafu wa kuuza nyumba za serikali nk.
Sisiem machoni na masikioni mwa wengi imekuwa chafu na imejaa wachafu. Uchafu wake unauona kila eneo, kwenye kura za maoni kuanzia serikali za mitaa (2014) na sasa udiwani, ubunge, hadi kiti cha urais ni ufisadi kwa kusonga mbele.
Ccm wote ni kambale tu ndani ya dimbwi, haiwezekani kambale mmoja awafanye wenzie sato wakati yeye mwenyewe angali kambale mwandamizi ndani ya dimbwi hilo hilo.
Rais wa Marekani Mh.Obama alipokuwa huko Ghana alinukuliwa akisema, AFRIKA HAIHITAJI MTU MWENYE NGUVU,AFRIKA INAHITAJI KUJENGA TAASISI ZENYE NGUVU. Maneno haya yana ukweli ccm kama taasisi yenye nguvu,nguvu za uozo na ufisadi inawabadili wasafi kuwa waovu na mafisadi.
Kwa ufupi, mh.Magufuli, kambale ndani ya dimbwi la kambale, hawezi badilika akawa sato wala hawezi kuwabadili kambale waliomzunguka kuwa sato.