Nani kama mama? Unampenda mama kweli?

Mkuu unamaanisha wababa huwa hawawapendi watoto wao kama kina mama?
wanaweza kuwapenda hata kuwazidi akinamama lakini hawawezi kuwajali kuwazidi akinamama,mama anaweza kuhangaika na mtoto mwenye maradhi ambayo wengi wa binaadamu tutamwogopa mtoto huyo lakini sio baba,mama atakomaa mpaka aone mwisho wa mwanae.vile vile ni mara ngapi umewasikia akina baba wakiwatoroka wakina mama kwa sababu labda ya kuzaa watoto tofauti.labda kilema au ana mtindio wa ubongo.mara nyingi wababa hukacha na kuwaaacha akina mama wakisota.mama ni mashine ya kuukamilisha mfumo wa uumbaji wa mwenyezi mungu viva mama popote mlipo ulimwenguni.
 
we acha tu. mama ni mama bwana. nakumbuka jinsi nilivyomnyea na kumkojolea sana maza nilipokuwa naanza kupata fahamu, aisee nilikuwa mlizi ajabu, nilimsumbua sana lakini alinipenda toka moyoni mwake.
 
Sawa mkuu,hapo nimekusoma vizuri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…