Nani kama Dr Slaa??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani kama Dr Slaa???

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Sep 23, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nani kama Dr. Slaa???


  Na tuweni wakweli? Katika wagombea URAIS bila kuangalia chama..ukiambiwa pigia kura "UADILIFU, HAKI na UZALENDO nani anastahili??? Jibu lako nani apewe uongozi wa nchi???  Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na
  mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili,
  tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni,
  wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na
  azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake
  popote pale walipo..  Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere
  kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini
  wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya
  wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani.

  Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge
  kupungzwa
  kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila
  woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa
  amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga
  kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?

  Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili
  ajibu bila unafiki!  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr
  Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana
  na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao
  Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa
  mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa
  ni nini?  Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma , Tabora,
  na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta
  mabehewa ambayo mababu
  zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi
  wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa
  vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na
  akina Carl Peters.  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni
  sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo
  lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata
  moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini,
  wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado!

  Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na
  vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni
  sehemu ya maisha yao . Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu
  ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na
  Tanzanite. CCM
  wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na
  wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya
  shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili
  ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji
  yao .  Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na
  CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa
  nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni
  Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa
  sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya
  walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba
  anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa
  sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba
  za mwalimu. Katika hotuba yake moja
  alisema waziri mmoja kule
  uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri
  alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule
  wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake.

  Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili
  imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara
  kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja
  mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia
  nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto
  utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata
  madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa
  chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa
  nguo njiani kwenda Mwanza,
  Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na
  Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya
  maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa
  kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya
  umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima
  wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao ? Nani asiejua asilimia 85 ya
  watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua
  tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi?

  Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni
  akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini
  wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa,
  anaweza
  kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa
  kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito , maziwa, national
  parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko
  maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi
  kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa
  nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika
  kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu
  haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi
  wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache
  woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona
  zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi,
  inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi
  wote na atuwekee katiba sawa. Huo
  ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi.

  CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio
  waendelee kututawala na kutunyonya.  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni
  kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu
  nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote
  zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe
  huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako
  wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu
  haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa
  waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
   
Loading...