Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,613
- 2,258
Habari wakuu?leo naombeni kwa pamoja tujadili umuhimu au ukuu wa baba ndani ya familia, mara nyingi nimekua nisikia watu wakihoji nani kama mama!? mara zote jibu langu huwa ni baba, kwanini? kwasababu yeye ndio kimbilio la familia nzima kuanzia mama hadi watoto, kwa kawaida mama huwa mwepesi kupokea taarifa za yeyote kwenye famillia, iwe shida,maombi,pendekezo au jambo jingine lolote, mama hujaribu kwa uwezo wake kuweka mambo sawa, iwapo likitokea lililo nje ya uwezo wake hulipeleka kwa baba bila kufikiria kama atalimudu au la, kwa baba ndio mwisho wa mtatizo yote, hastahili kushindwa, mama yupo kwa niaba ya baba, iweje tena awe zaidi ya anaemwakilisha? karibuni wakuu,weledi, tujadili kwa hoja.