Nani huumizwa zaidi kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke?

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,638
4,522
Kama mada inavyojieleza. Sote huwa tunaumia tunaposalitiwa na wapenzi wetu. Utakuta nimemgharimia kumsomesha, kumsubiri amalize masomo na kuhakikisha anaishi bila ya matatizo. Anapomaliza bila aibu ananiambia wewe sio type yangu wala hukuwa chaguo langu .Kama gharama sema ni kiasi gani nikurudishie. Ukija upande wa pili nao utakuta msichana amemvumilia mwanaume toka hana kitu akampa upendo wa kweli na kumfariji mpaka mwanaume anafanikiwa kimaisha. Inapofikia wakati wa kuoa utasikia wewe hukua chaguo langu au wazazi wangu wamenitafutia mke kijijini. Hapa wote wawili mwanaume na mwanamke tunaumizwa. Sasa swali langu ni nani kati ya mwanaume na mwanamke anayeumia zaidi pale anapotendwa kwenye mahusiano? Na ni jinsia ipi inayoongoza kwa kuumizwa na wenzi wao? Binafsi niliumizwa na mrembo mmoja nikaapa kutopenda tena na nikaamua maisha yangu yatakuwa ya ulevi tu.
 
Inategemea.

Hapa jinsia haihusiki hata kidogo.

Kwasababu kuna jinsia ya KIKE waliyojitoa kwa MAPENZI ya DHATI, kwa HALI na MALI na matokeo yake wameambulia MAUMIVU makubwa
 
Inategemea.

Hapa jinsia haihusiki hata kidogo.

Kwasababu kuna jinsia ya KIKE waliyojitoa kwa MAPENZI ya DHATI, kwa HALI na MALI na matokeo yake wameambulia MAUMIVU makubwa
Jinsia inahusika mkuu. Swali linataka kujua nani anaumia zaidi. Nikimaanisha kuwa kati ya me na ke nani mwenye uwezo wa kuvumilia maumivu ya kutendwa??
 
Yoyote yule ampendaye mwenzake kutoka moyoni atakapomsaliti lazima aumie awe me au ke...maumivu hayanaga jinsia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona swali halijaeleweka. Nataka kuuliza ni nani anayehisi maumivu zaidi. Kwa mfano kati ya me na ke nani hufurahia zaidi tendo la ndoa? Kwa hiyo swali langu limelenga kutazama anayeumia zaidi kwa kuangalia reaction ya mtu baada ya kutendwa ??
 
Jinsia inahusika mkuu. Swali linataka kujua nani anaumia zaidi. Nikimaanisha kuwa kati ya me na ke nani mwenye uwezo wa kuvumilia maumivu ya kutendwa??
Kiongozi Wangu.

Ndio maana nikasema inategemea.

JINSIA haihusiki linapokuja kwenye Suala la kutendwa.

Ndio maana kuna mwingine akitendwa anaweza kufanya tukio moja la Hatari na Mwingine akaamua kusamehe na kusahau.

Kivipi?

Mwingine akitendwa, usishangae akaja kuchoma Nyumba MOTO, au kumuwekea SUMU aliemtenda, au kufanya tukio lolote lile la KIKATILI/KINYAMA.

Au hata kumfyatulia RISASI aliemtenda.

Sasa linapokuja Suala la kufanya tukio lolote la Hatari ujue hapo haijalishi kama anaefanya tukio hilo ni wa jinsia ipi/gani.

Hapo inategemeana na Muhusika mwenyewe, na wala si jinsia
 
Nmesoma heading tu.

Katika.mapenzi mwanaume na mwanamke wote huumia ila itategemea uzito wa mapenzi na Timing ya kuacha/kuachwa.

Ushauri, Ukishaona kiashiria ambacho hatima yake unaijua, jitoe fasta kabla ye hajakuwah, yaan hata km unampenda wee jitoe alafu lazimisha moyo nakili vijue mmeachana...

Tuache masiala mara mia Uache mmeshakulana ,kuliko kuachwa mmeshakulana
 
Kiongozi Wangu.

Ndio maana nikasema inategemea.

JINSIA haihusiki linapokuja kwenye Suala la kutendwa.

Ndio maana kuna mwingine akitendwa anaweza kufanya tukio moja la Hatari na Mwingine akaamua kusamehe na kusahau.

Kivipi?

Mwingine akitendwa, usishangae akaja kuchoma Nyumba MOTO, au kumuwekea SUMU aliemtenda, au kufanya tukio lolote lile la KIKATILI/KINYAMA.

Au hata kumfyatulia RISASI aliemtenda.

Sasa linapokuja Suala la kufanya tukio lolote la Hatari ujue hapo haijalishi kama anaefanya tukio hilo ni wa jinsia ipi/gani.

Hapo inategemeana na Muhusika mwenyewe, na wala si jinsia
Duh hapo nimekuelewa mkuu. Naomba experience yako japo moja tu ya kutendwa.
 
Duh hapo nimekuelewa mkuu. Naomba experience yako japo moja tu ya kutendwa.
Kiongozi.

Kama nikipata Muda nitarudi tena baadae.

Nikikosa Muda basi Kesho hiyo tena.

Maana nimetingwa na Shughuli nyingine za kufanya.

Napenda sana ningekuwa na Muda wa kutosha hapa ili tupate kupeana japo Machache
 
This is not a competition where one has to win
It's a love between a husband and a wife
not between Bruce Lee and Chuck Norris
(Bruce, Bruce, Bruce)
It's also not a boxing clash where one has to be knocked out
It's a love between a husband and a wife
Not between Ali and Foreman

FALLY IPUPA

You said it well bro. But it is not love that we are talking about rather the pains of betrayal.
 
Back
Top Bottom