Watanzania wote tuko tayari kutoa maisha yetu kwa ajili ya taifa na wala sio katika kutafuta vyeo. Tumefanya hivi, tunafanya na tutaendelea kufanya kwani ni jukumu letu.
Kelele unazozisikia sio za kuzuia kupambana na biashara ya unga bali ni njia uliyotumia.
Halafu nikushauri ndugu yangu, sasa hivi vita inayoendelea sio ya unga tena bali ni ya bangi, kwangu mm kupambana na bangi ni kuwaonea wavutaji wakati wavuta sigara wako mitaani wanavuta.
Ukiniambia unapambana na unga nitakuelewa maana unga una madhara ya dhahiri na sio bangi.