Nani ataongoza kampeni za Magufuli?

Nani ataongoza kampeni za Magufuli?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Kumpigia mtu kampeni ili akubalike kwa wapiga kura sio jambo dogo kulifanya, linahitaji mpiga debe aliye msafi na anayekubalika kwa wapiga kura. Mpiga debe hana budi kuwa na rekodi nzuri na msafi wa nje na ndani. Je CCM nani anafaa kuongoza kampeni za kumnadi Magufuli kwa wapiga kura?
 
Njia na Mawazo ya Wanadamu ni tofauti na Utendanji wa Mungu.Uteuzi wa Dk.John Magufuli si wa Wanadamu,bali ni wa Mungu.
 
Attachments

  • DK John Magufuli.JPG
    DK John Magufuli.JPG
    56.7 KB · Views: 631
Kumpigia mtu kampeni ili akubalike kwa wapiga kura sio jambo dogo kulifanya, linahitaji mpiga debe aliye msafi na anayekubalika kwa wapiga kura. Mpiga debe hana budi kuwa na rekodi nzuri na msafi wa nje na ndani. Je CCM nani anafaa kuongoza kampeni za kumnadi Magufuli kwa wapiga kura?
Kangi Lugola na Deo Filikunjombe
 
Acheni utani sasa, huyo aliyemaliza mlimwita hivyo baadae mkaanza kukana hamkumwita chaguo la Mungu. Hata awe nani CCM hawawezi kuleta mabadiliko nchi hii, na akichaguliwa huyu ni miaka mingine 10 ya maumivu kama si mitano.
 
Tatizo watu wamelogwa na CCM sioni huyu kama atatutoa tulipo
 
Lukuvi,filipolunjombe,mwakyembe, makongoro au olesendeka, kange lugola,january,mwiguli, Asha migilo,Anakilango,

hawa wote wategeneze timu moja,
 
Kampeni itaongozwa tu, hata kama haitamfikisha Ikulu
 
Kama atajikita umaliziwadi wa mchakato wa katiba pendekezwa utamgharimu magufuli sana. Labda awahakikishie watanzania kwamba ataanza mchakato kwa kuheshimu naoni ya tume ya jaji warioba.
 
Kila mwana CCM awe fisadi asiwe lazima atapiga tu kampeni maana hamuna namna nyinngine sasa.
 
Magufuli wala mtu yeyote ndani ya ccm hataweza kwenda kinyume na ccm. Hiyo katiba ni ya ccm na ilichakachuliwa na wanaccm Magufuli akiwemo wala hakuonyesha uchungu wala upinzani wowote juu ya fujo zilizokuwa zikifanywa na wanaccm na yeye akiwemo. Leo unategemea abadilike na kusimama na wannachi? Sahau.

Akisema, ataongea kwa kuwaridhisha lakini amini usiamni. The moment anakuwa raisi, kura ya maoni inapigwa na kurasimisha uozo ule kuendesha nchi ii maslahi yake na waliomweka madarakani yalindwe!.

Kutegemea Magufuli kusimama kinyume na ccm ati awe upande wa wananchi, ni sawa na KUTEGEMEA SAMAKI ASOGEE KUCHOCHEA TANURU LA MOTO!.

Hope umeelewa.

Kama atajikita umaliziwadi wa mchakato wa katiba pendekezwa utamgharimu magufuli sana. Labda awahakikishie watanzania kwamba ataanza mchakato kwa kuheshimu naoni ya tume ya jaji warioba.
 
Back
Top Bottom