Nani ataichagua CCM?

Nani ataichagua CCM?

Hakikwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2010
Posts
4,049
Reaction score
1,022
Je ni nani atakaye ichagua CCM kwa sasa? Hivi Watanzania tumesahau ya CCM iliyotutendea mpaka sasa? Naomba niwakumbushe haya yaliyofanyika chini ya uongozi imara wa CCM.
1. Kuuzwa kwa mgodi wa Kiwila kwa bei ya kutupwa.
2. Utoroshaji wa Wanyama pori.
3. Ujangili wa kupindukia wa tembo.
4.EPA
5.ESCROW
6.MEREMETA
7.RICHMOND
8.Ununuzi wa RADA isiyoendana na bei halisi.
9. Mikataba mibovu ya madini.
10.Ufujaji wa pesa za umma.
11. Deni la taifa kupaa kwa kasi.
12. Mfumuko wa bei za bidhaa wa kupindukia.
13. Huduma mbovu za afya na elimu.
14.Kuuawa kwa viwanda vingi.
15. Ukosefu wa ajira
16. Matumizi mabovu ya raslimali
17. Rushwa iliyokithiri kila sekta.
18. Kutelekeza shughuli za kilimo na ufugaji.
Je Mtanzania mwenye uelewa na uchungu na taifa hili utaichagua CCM kwa lipi? Wakati umefika wa kuipumzisha CCM hili halipingiki labda kama tumelogwa. Sioni dhamira ya CCM kumkomboa Mtanzania zaidi ya hadaa tupu. Mtanzania chukua hatua ukomo wa CCM umefika.
 
Mimi na wewe, pamoja na wasiokuwa wachagga, na UKAWA original. CCM itashinda nyie mko wachache.
 
Hapa wenzio umeme umekatika saa 12 na robo, hapo ndio nitolee hadi jioni au kesho asubuhi. Kwa style hii ya mgao wa umeme nani anaichagua CCM
 
Mimi na wewe, pamoja na wasiokuwa wachagga, na UKAWA original. CCM itashinda nyie mko wachache.

Unanufaika na mfumo wa ccm vinginevyo waonee huruma wengine. Tuichague ccm kwa lipi hasa. Pia unaukabila ndani yako
 
Hivi kweli wapanga kampeni wa ccm hawajui kama mgao wa umeme unamharibia mgombea wao. Au ndio wameamua tu kumtoa sadaka mzee wa watu asipate kura hata asilimia kumi
 
Unanufaika na mfumo wa ccm vinginevyo waonee huruma wengine. Tuichague ccm kwa lipi hasa. Pia unaukabila ndani yako

Ndio maana ya demokrasia, wewe unachagua hiki na wengine wanachagua kile halafu tunahesabu kura mshindi anapatikana
 
Wale wezi wa escrow, na watoto wa makada ambao ni wanufaika kwenye mashirika yetu ya umma na wakwepa kodi ili kulinda uhai wao wa kifisadi uendelee.
 
Mimi na wewe, pamoja na wasiokuwa wachagga, na UKAWA original. CCM itashinda nyie mko wachache.

ACHA DHANA OVU!/
ACHA UMUFILISI WA FIKRA!
ACHA UKABILA!
->>usipandikizwe uovu na waovu na walafi,wanaojiona wao tu pekee ndio wanaostahili!
 
Mtu yeyote anayeipenda Tanzania hawezi kumkabidhi Mtei na ukoo wake kupitia hicho kitega uchumi cha chaggadema.
 
ACHA DHANA OVU!/
ACHA UMUFILISI WA FIKRA!
ACHA UKABILA!
->>usipandikizwe uovu na waovu na walafi,wanaojiona wao tu pekee ndio wanaostahili!

Usipanic ukweli ni ukweli tu, angalia groups zao FB ndio utakubaliana na mie. Hakuna uovu kusema ukweli CCM utapata kura.
 
Hivi kweli wapanga kampeni wa ccm hawajui kama mgao wa umeme unamharibia mgombea wao. Au ndio wameamua tu kumtoa sadaka mzee wa watu asipate kura hata asilimia kumi
Hakuna kitu hapo, maneno tu hayo hata kwenye khanga yapo, CCM itapigiwa kura na wazalendo na werevu tu
 
Usipanic ukweli ni ukweli tu, angalia groups zao FB ndio utakubaliana na mie. Hakuna uovu kusema ukweli CCM utapata kura.

Facebook haipigi kura watanzania Ndio watapiga kura, angalia % ya watanzania wanaotumia Facebook, tweets, na website.
UKAWA mtapigwa asubuhi na mapema usidhani watanzania wamesoma sera zenu kwenye website.
 
Hapa wenzio umeme umekatika saa 12 na robo, hapo ndio nitolee hadi jioni au kesho asubuhi. Kwa style hii ya mgao wa umeme nani anaichagua CCM

Hapa kwetu ulikatika saa tano usiku, kuuona tena hadi jioni, nani awachague? Umeme hautoshi hadi tuna gawiwa kwa miaka sasa. Hata huo kidogo bei yake ni kubwa mno.
 
Facebook haipigi kura watanzania Ndio watapiga kura, angalia % ya watanzania wanaotumia Facebook, tweets, na website.
UKAWA mtapigwa asubuhi na mapema usidhani watanzania wamesoma sera zenu kwenye website.

Yaani hapa uko pamoja na mie
 
kama nyie mnavosema mtachagua hata kama gonjwa, nasi ccm tuna mahaba nayo tunaichagua hata upige mipasho yako

Hakikwanza
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom