tHe NapSTer of Tz
Member
- Mar 30, 2007
- 86
- 1
mumeshawahi kuona movie inaitwa THE INTERPRETER?
ni movie nzuri ambayo inaelezea jinsi viongozi wanapokua njee ya madaraka na kukusanya watu na kusema anapigania haki na maslahi ya watu! na then akipata madaraka na yeye anakuwa worst of worsts!... watu wengi wanaogopa changes!
most of them people wanaogopa changes in regimes kwasababu inaambatana na visasi!.... usiongelee kuhusu mapinduzi lazima uelewe damu za ndugu zetu wa visiwani waliopotea wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi!!...
mumeshawahi kuona movie inaitwa THE INTERPRETER?
ni movie nzuri ambayo inaelezea jinsi viongozi wanapokua njee ya madaraka na kukusanya watu na kusema anapigania haki na maslahi ya watu! na then akipata madaraka na yeye anakuwa worst of worsts!... watu wengi wanaogopa changes!
most of them people wanaogopa changes in regimes kwasababu inaambatana na visasi!.... usiongelee kuhusu mapinduzi lazima uelewe damu za ndugu zetu wa visiwani waliopotea wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi!!...
Nakubali kwamba njia ni mapambano lakini si ni lazima mapambano yenyewe yaongozwe na itikadi ambayo iko wazi na inayoeleweka kwa wale walio mstari wa mbele na wale wanaohamasishwa kujiunga na mapambano yenyewe?
Pengine moja ya sababu kubwa zinazotufanya baadhi yetu kushindwa kushiriki kikamilifu katika mapambano ni kukosekana kwa itikadi ya mantiki ya mapambano yenyewe. Si kila anayeshiriki katika kuifia dini anakuwa anayo itikadi inayomsukuma kufanya hivyo?
Siri kubwa ya wananchi kushinda ni kuelimika.
Vyombo mbalimbali vya habari kama REDIO, TVS, MAGAZETI NA mitandao ya
internet, kama JF, ni silaha kubwa sana kwa watanzania...Kwa mfano halisi,
mimi binafsi nimepata mtazamo-hasi baada ya kukutana na website hii!!!!
Imenibadilisha, NIMEKUWA MPIGANIA HAKI NA USAWA...
Je kule kwenu GUNGULUGWA wana silaha kama hizi?
Shime sote, na kila mtu kwa nafasi aliyo nayo, aanzishe mapinduzi ya
UKOMBOZI WA AKILI.
Inkosikazi.. katika vita ambapo adui amekuzidi kwa idadi, ubora wa silaha na zana za kivita mikononi mwako una vitu vichache sana vya kukusaidia.. the most important one is timing.. so.. timing here is everything..
Naam, umenena.
umefika wakati wa kutoka kwenye internet, Magazeti, TV, Radio, n.k. na kuunda kikosi cha 'ukombozi' cha kwenda vijijini kuelimisha na kuhamasisha wananchi! Wapigania Uhuru wa nchi yetu walikuwa si wasomi kama walivyo wengi humu lakini waliweza kwenda vijijini kuwahamasisha wananchi na kuikomboa nchi kutoka kwa Wakoloni Wazungu wenye elimu na mabavu. Iweje wasomi wa zama hizi washindwe?
Tutoke kwenye internet!
Mimi naamini kwamba bila ya kuwa na itikadi ya wazi itakuwa ni vigumu sana kuendesha mapambano kwa sababu wapiganaji wanahitaji kujua falsafa gani inayowaongoza katika mapambano yenyewe na ni nini hatima ya kile wanachokipigania.
So, I believe kama tutangeneza ideology haiwezi kuwa ideology without specificities.. it is has to be an ideology that is sensible, reasonable and more than that it has to be an ideology that is believable and leads to clear achievements. Haiwezi kuwa itikadi ya vitabuni.
oh! I get the point of the thread...
hey.. mwenzetu ulikuwa wapi? stop hacking and start checking..
Tofauti ya maisha kati ya watawala na watawaliwa imeongezeka zadi.tatizo ni kwamba kuna ile mentality ya kwamba thats the way it should be.Nadhani wapiga kura wengi ni wakulima na wanavijiji ambao hawaelewi?Nataka sana kujua demographic ya wapiga kura wa Tanzania.Ningependa sana kujua ni kina nani hao wanaotuchagulia viongozi kwa wingi wao.Hivi ni kweli hao wananchi wana furaha kiasi cha kuirudisha ccm madarakani all the time kwa ushindi wa kishindo?Kwanini tunaona umma unajitokeza kwenye mikutano na maandamano,je umma huo hujitokeza kwenye kupiga kura?
Ni mgongano wa kihistoria ambao ulipaswa kutokea. Ni mgongano ambao hutokea mahali popote panapokuwa na tofauti kubwa kati ya watawala na watawaliwa. Ndivyo ilivyokuwa kwenye Mapinduzi ya Ufaransa, Mapinduzi ya Marekani na Mapinduzi ya Bolshevik (Urusi).
Ni yale yale yaliyotokea na kusababisha mapinduzi ya Cuba yaliyomuingiza Castro madarakani. Ndiyo! Ni yale yale yaliyotokea pia kwenye mapinduzi ya Zanzibar!
Migongano ya namna hiyo asili yake mara zote ni pale wananchi wanapotambua kuwa hawana usawa na watawala wao na ya kuwa tofauti ya maisha yao na yale ya watawala ni kubwa mno na ya kwamba mwananchi wa kawaida anajikuta hana nafasi yoyote aidha ya kufanikiwa au ya kuweza kuishi maisha yenye utu, usawa, haki na heshima.
Nchi chache zimeweza kupitia mgongano huo kwa njia ya nguvu (kama mifano niliyotoa) au kama ilivyotokea huko Ukraine na Georgia miaka ya karibuni kwa njia ya nguvu ya umma.
Tanzania yetu inapitia mgongano huo katika hatua zake za awali. Silaha ambayo wananchi wanatumia leo hii ni nguvu yao ya hoja na wanatarajiwa kubadilisha serikali yao kwa nguvu ya kura.
Hata hivyo hilo halitakuwa rahisi kwani dalili yote inaonesha kuwa watawala hawako laini kuruhusu mabadiliko makubwa ya kiutawala yenye kupendelea wananchi wa kawaida. Hivyo, mgongano unaendelea. Swali ni nani ashinde? Na ni nani ataamua mshindi!?
Nisikilize:
[mp3]http://mwanakijiji.podomatic.com/enclosure/2009-04-29T23_41_36-07_00.mp3[/mp3]