Donyongijape
JF-Expert Member
- May 28, 2010
- 1,497
- 815
NI KODI YA JENGO. NIMEISIKIA LEO ILA BADO SIJAIELEWA
Je,hiyo ni tofauti na kodi ya ardhi tunayolipa kila mwaka?Kodi ya MAJENGO ni kodi inayotozwa kwa mmiliki wa jengo la makazi au biashara... jengo hilo ufanyiwa tathimini na kutoa kodi yko...
KAMA UNAWAPANGAJ WALA USIWAZEHabari wanabodi.
Hivi karibuni nimepata Hati ya Madai ya Kodi ya Jengo kwa Mwaka 2015/2016 ya kibanda changu ambacho kina umri wa mwaka mmoja. Eneo langu halina HATI (TITLE DEED) ni mikataba tu ya kuuziana eneo.
Sasa ningependa kujua kutoka kwa Manguli wa Sheria au Wenye uzoefu humu JF, je hata Mimi natakiwa kulipa hio kodi ya Jengo ilihali sijapata Title Deed na hakuna report yoyote inayoonyesha value ya Nyumba yenyewe zaidi ya kiwango kilichoandikwa kwenye hio hati ya Madai (Demand Notice)?.
Naomba msaada tafadhali. Ningetamani mnifafanulie zaidi, ikiwezekana na vifungu vya sheria.
Asanteni sana.
0.15% *thamani ya nyumba, je kwa bajeti hii mpya si kuna mabadiliko? kwa mwaka tutatumia calculation zipi kupata kodi ya jengo......,na nyumba yangu mpaka nianze kuchajiwa kodi ya jengo ni masharti gani ni lazima niyatimize kuanza kulipa kodi ya jengokama unamiliki jengo lolote lazima ulipe kodi na kodi unayotakiwa kulipa ni 0.15% ya thamani ya jengo ila wakadiriaji kodi wanatabia ya kuweka kodi kiwango cha juu hapo itabidi mpambane ikiwezekana mtathimini aitwe ili kupata thamani halisi ya jengo
Kwa bajeti hii hakuna kilichobadilika ila kwa nyumba ambayo haijafanyiwa tathimini ya chini watachaji 10,000/= na ghorofa watachaji 50,000/= lakini kwa zile zilizofanyiwa tathimini gharama itabaki ileile 0.15% ya thamani ya nyumba0.15% *thamani ya nyumba, je kwa bajeti hii impya si vitu vimebadilika, kwa mwaka tunatumia calculation zipi kupata kodi ya jengo......,na nyumba yangu mpaka nianze kuchajiwa kodi ya jengo ni masharti gani ni lazima niyatimize