Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Nimesoma maoni-kauli mbalimbali kuhusu Ripoti ya Kamati ya Prof. Mruma juu ya mchanga wa dhahabu iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli.
Kimsingi,watanzania kwa mamilioni yetu,akiwemo Wakili Msomi na Mbunge Tundu Lissu pamoja na wengineo wenye mawazo kama yake,tunakubaliana kuwa Rais ana nia njema.
Tunakubaliana kuwa Rais analinda rasilimali zetu kwa ajili yetu na tupo naye pamoja. Kuna kukubaliana kuwa Rais anafanya kazi ngumu kwakuwa sheria na mikataba ya madini haijakaa sawa
Lissu na wenye mawazo kama yake wamejaribu kutoa tahadhari. Tahadhari za kisheria katika kuvunja au kuathiri mikataba ya madini kati ya Tanzania na wawekezaji wengine. Lissu na wenzake hawajawahi kutamka kumpinga Rais wala kupinga ulindwaji wa rasilimali za taifa
Hakuna mahali ambapo Lissu anazuiwa kutoa mawazo yake juu ya lolote lihusulo taifa letu. Ripoti ya Kamati ya Prof. Mruma imejadiliwa ipasavyo na wanasiasa,wafanyakazi,wafanyabiashara na wananchi wa kawaida. Hadi Mtemi Chenge,Werema na Dr. Kilangi wametoa maoni yao
Kwanini na nani anapotosha maoni ya Lissu na wenye mawazo kama yake? Kwa faida ya nani? Kutoa tahadhari si kupinga wala kuwatetea wawekezaji. Hakuna haja ya kupotosha hata mambo ya kitaifa.