Nani Anapakumbuka Hapa?

Hapo ilikuwa ni just few meters kutoka ofisi yangu ya zamani, Kinondoni Road. Some bomb particles zilirushwa mpaka ofisini kwetu na vioo vya jengo letu vyote vilipukutika!!! Usicheze na hiyo kitu inaitwa Bomu!!!!

Tiba
 
Nilikuwa kwenye mataa ya hapo Kenyatta...mkoko wangu ukapaajuu kutua chini hamna hata kioo kimoja! Miwani ndio iliniokoa kupofuka
 
....Ni Tendo la kusikitisha lisiloweza kusahaulika ... aslan
 
Siku hiyo nilikuwa Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam, nikielekea kazini. Yaani kishindo cha mlipuko kilikuwa ni balaa. Sikujua nini kimetokea mpaka nilipofika kazini ndipo nilipofahamu kuwa Osama ametutumia salamu.
 
Sintaisahau hiyo siku,nilikuwa Kiria Bar nakunywa supu
 
Nilikuwa naandika insha ya haki za binadamu kukumbuka miaka 50 ya Human Rights (UNO)
 
Nilikuwa na mke wa mtu nilishituka nikazani ndio nimefumaniwa!!!!!!!!!!!
 
tumemiss tukio kama hili siku nyingi sasa
 
Umenikumbusha mbali sana aisee! Sitaisahau hiyo siku
 
Sisahau siku hiyo nilikuwa kwa Mama PS pub kama saa nne nilisikia kishindo mara nikaona vyuma vikubwa vinatoka angani nikasema labda ndege imedondoka nini kuchungulia naona mshikemshike barabarani gofu,ultmate nikajua ubalozini kimenuka mara jamaa anasema fungulieni itv cnn wanaonyesha na kenya pia kimenuka! Osama alikuwa noma!
 
Bongo ni Zaid ya burdaan, Kila mtu anajifanya alikuwa karibu na eneo la Tukio, naskia askari wa kitasha walikuwa wanawahi Maiti za kizungu na kuacha majeruhi weusi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…