Ccm ijitahimini. Mmeharibu nchi,wanaotajirika ni wale tu wachache wanaopewa nafasi. Lakini wananchi walio wengi bado ni masikini sana.
Ukipita vijijini huko watu wanatia huruma. Zamani watu walikuwa wanategemea walau kilimo kiwalishe,lakini siku hizi ardhi imeharibiwa kwa tabia za nchi kilimo chochote siku hizi lazima kitumie mbolea. Ni wachache wenye uwezo wa mbolea. Kilimo siku hizi lazima uwe na pesa pia.
Miaka kumi tu hapo mbele nchi hii kwa mwenendo huu itakuwa na watu masikini kuzidi. Huku nyie ccm mkifanya mambo yoyote ya Umma yakienda vibaya mnawasingizia wapinzani. Na bahati mbaya hata bungeni hawamo. Sasa hizo Sera za wapinzani zinatoka wapi?.