Nani anamdai Marehemu Lemutuz?

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
21,515
41,977
Katika jambo ambalo naona haliko sawa hadi leo ni suala la Kuanza kutaja madeni ya marehemu msibani kama kuna mtu anamdai why asiifate familia kumtunzia heshima marehemu?

Kwenye msiba wa Lemutuz yule Pinto anasema nyumba aliyokuwa anaishi lemutuz ni yake hata Gari noah alimuazima sio ya Lemutuz Why tunawavua nguo marehemu?

Sio utamaduni mzuri nadhani hili inabdi lipitiwe upya na kurekebishwaa.

Binafsi kuna msiba fulani wa Ndugu yangu jamaa wa karibu sana ambae kiukweli alisimama hadharani kuanza kutaja kiasi anachomdai Marehemu toka siku ile nilimshusha sana vyeo na kuona hajitambui maana kama familia angetufata sidhani kama tungekataaa.
 
Huwa munampa sifa Sana huyo jamaa aliyekulia nyumba ya mboga nne ugali robo
hakuna kijana yeyote tanzania ambaye anaweza fanana na

Lemutuz​

Lemutuz​

jamaa ni shujaa ambaye hata story yake ya maisha naweza kuwa hadithia wanangu na nina hakika wataipenda

chukua maua yako Mkuu mungu akuweka mahali safi sana
Sijaona ushujaa wowote labda km watz ni wajinga , ushujaa wa kula bata mjini huku akiwa na back up ya mzee wake!!

Pia anatajwa kuwa ni Njagu msela ..

Acheni akina Malcolm X wabaki na ushujaa ..Bongo michosho Sana.
 
Huwa munampa sifa Sana huyo jamaa aliyekulia nyumba ya mboga nne ugali robo

Sijaona ushujaa wowote labda km watz ni wajinga , ushujaa wa kula bata mjini huku akiwa na back up ya mzee wake!!

Pia anatajwa kuwa ni Njagu msela ..

Acheni akina Malcolm X wabaki na ushujaa ..Bongo michosho Sana.
mimi na wewe hatuwezi fikia hata nusu ya huwezo wa huyu jamaa Mkuu
 
Lazima ijulikane anayemdai na anayedaiwa na Marehemu kubwa ni deni lilipwe ili Marehemu apumzike kwa Amani.... Pinto yupo sahihi asingesema kuhusu vitu vyake angevipataje ndugu si wangeingiza kwenye mali za marehemu?

Ishi huku ukijua utakufa muda wowote usijisahau kama vile utaishi milele wakati haiwezekani.
 
Huwezi kuzika maiti inayodaiwa madeni wanaomdai wanajitokeza hadharani ila sio kutaja maana wanaenda kuongea na wana wafamilia.

Ila kwa sisi waislamu lazima maiti kabla ya kuzikwa kama kuna wanaomdai wanaenda kuonana na familia yake.

Ila kila mara inasisitizwa tena sana mno watu wasamehe ili marehemu apate kupumzika ..Hekima ya hii **** kiwango ambacho kama mtu anaidaiwa ni kikubwa basi ataachia familia yake msala sasa ndo ukute watoto wadogo au ndugu hawana kitu ...
 
Katika jambo ambalo naona haliko sawa hadi leo ni suala la Kuanza kutaja madeni ya marehemu msibani kama kuna mtu anamdai why asiifate familia kumtunzia heshima marehemu?

Kwenye msiba wa Lemutuz yule Pinto anasema nyumba aliyokuwa anaishi lemutuz ni yake hata Gari noah alimuazima sio ya Lemutuz Why tunawavua nguo marehemu?

Sio utamaduni mzuri nadhani hili inabdi lipitiwe upya na kurekebishwaa.

Binafsi kuna msiba fulani wa Ndugu yangu jamaa wa karibu sana ambae kiukweli alisimama hadharani kuanza kutaja kiasi anachomdai Marehemu toka siku ile nilimshusha sana vyeo na kuona hajitambui maana kama familia angetufata sidhani kama tungekataaa.
Aisee nimemsikiliza yule kaka kanishangaza🤔
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea Yale pale Kwenye kadamnasi?
Si angewafuata familia tu ?
Mpk nikaona Kuna watu km 3 hivi wanamfuata km walikuwa wanamnong'oneza aache kuongea hivi ,aisee kanishangaza sn
 
Huwa munampa sifa Sana huyo jamaa aliyekulia nyumba ya mboga nne ugali robo

Sijaona ushujaa wowote labda km watz ni wajinga , ushujaa wa kula bata mjini huku akiwa na back up ya mzee wake!!

Pia anatajwa kuwa ni Njagu msela ..

Acheni akina Malcolm X wabaki na ushujaa ..Bongo michosho Sana.
Amekula wapi mboga 4? 😅 Aisee laiti ungejua hata hayo maisha hajayaonja kaishi Kwa tabu usingesema!
Haya mambo yasikie tu aisee
 
Aisee nimesikiliza yule kaka kanisjangaza
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea yake pale Kwenye kadamnasi?
Mpk nikaona Kuna watu km 3 hivi wanamfuata km walikuwa wanamnong'oneza aache kuongea hivi ,aisee kanishangaza sn
Yani haina faida yoyote sababu hata angewafata ndugu private sidhani kama wangekataa..
 
Amekula wapi? 😅 Aisee laiti ungekua hata hayo maisha hajayaonja kaishi Kwa tabu usingesema!
Haya mambo yasikie tu aisee
Kuna muda huwa tunapishana na wazee halafu ukute mzee Ni mtata na anamkwanja anaamua kukupitisha kwenye tanuru la Moto ,akili ikitulia anaamua kukuinua ,,,Le ni kama vijana wa mjini tu aliyeamua kuishi maisha yake na mzee malecela akaamua kumuacha apendavyo...Kuna upande wa simulizi hatukupata scene.
 
Yote yanawezekana, mkuu ..
ila Kwa jinsi hata ndugu wa kuzaliwa walivyokuwa wanamtenga ,hapana aisee! Mpk kwenye misiba khaaa🙌! Too much hatred! Tena huyo aliyeongea kuhusu vitu vyake Kuna kitu aliongea aisee,kuhusu marehemu dada ake ,🤔nilishangaa sn!mpk unajiuliza walikuwa wanamchukia kaka Yao kiasi hiki? walimtenga mno, ,yule kaka hajawahi kupata upendo kabisa ,sio Kwa familia mbaya zaidi sehemu iliyobaki peke ilikuwa Kwa mke Nako akaangukia pua!Ndo maana alipata hata shida ya moyo....
 
Pinto aliongea vile kudai mali zake au kuelezea maisha ya marehemu?Binafsi sikupendezwa sababu ni kama kumvua nguo marehemu.Mimi nisimame kwenye msiba wa rafiki yangu nianze kusema "Ooh kuna wakati alikuwa hana hata sumni mimi ndio nikampatia"Hapana kwakweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom