Nani Analipa Gharama za Kikwete za Kampeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani Analipa Gharama za Kikwete za Kampeni?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bobby, Aug 23, 2010.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Habari wana JF!

  Sorry, kuna kitu kinanisumbua kidogo. Nimejaribu kufuatilia safari za jk kwa ajili ya kampeni sijaona tofauti yeyote kimuundo na kigharama kati ya safari za kawaida anapokuwa rais na hizi za sasa anaposafiri kwa ajili ya kampeni kama mwenyekiti na mgombea wa urais kwa ticketi ya ccm. Mfano ni safari ya Mwanza ambayo picha zinaonyesha ni ndege ya serikali ilitumika, swali ni nani alilipa gharama za hiyo ndege kwenda Mwanza na gharama zinginezo kwa ajili ya kampeni za ccm? Je ni kodi zetu watanzania kwa maana ya wana CUF, CHADEMA, TLP au wanachama wa chama chochote na hata wale wasio na vyama zinatumika kumnadi mgombea wa ccm?

  Mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kwamba hakuna hata safari moja ya kampeni yenye manufaa kwa Taifa, safari zote ziko meant kuomba ridhaa ya watanzania kuendelea "kuitawala" nchi hii. Nionavyo mimi ni makosa kwa kodi za watanzania kutumika kwenye kampeni za chama chochote kile iwe ccm au chama kingine chochote. Nina mifano ya nchi kadhaa Africa, Ghana ni miongoni mwao ambao wamefanikiwa kutofautisha kampeni na shughuli zingine za rais. Kwa Ghana kwa mfano, endapo waziri anateuliwa kugombea urais anatakiwa kuresign kwenye nafasi kama waziri ili aweze kushiriki kwenye kampeni. So ni kitu kinachowezekana kama tukiamua. Hapa kwetu sivyo, jk aliendelea kuwa waziri mwaka 2005 pamoja na kwamba hakufanya kazi kwa zaidi ya miezi miwili kwa ajili ya kampeni. Wajuvi kwenye hili naomba mnisaidie, inanikera tena sana kwa kodi yangu kutumika visivyo kwenye kampeni ya kupeana tshirts ili hali tumboni nina njaa ya siku mbili an mm si mwanachama wa chama chochote kile nchini.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama utaratibu utafuatwa, CCM ndio wanapaswa kulipa hizo gharama. Kuhusu matumizi ya ndege ya serikali inalipiwa pia. Hata kama Lipumba au Dr Slaa atapenda kuitumia ataikodi kama ambavyo CCM wanaikodi.
   
 3. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  wakuu hapa tunadanganyana yaani ni kama kuhamisha hela kwenye mfuko wa shati na kutia wa suruali.twawezaje kupima kama wanalipa na si kiini macho?ila hapa ndipo nakumbuka kuwa kumbusha watawal wetu MSITUONE WAVUMILIVU MKUHISI HATUHISI MAUVI!
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm inaendesha kampeni kwa pesa zake yenyewe, kutoka kwenye ruzuku ya mwezi ya serikali kwa chama hicho, inaendesha kampeni kwa hera za wanachama wenye mapenzi mema, pia inaendesha kampeni kupitia makundi ya mafisadi, hasa wahindi , hawa wanajitolea vitu kama mafuta ya diesel, wanajitolea magari ya kusafirisha mamia ya wapenzi, mashabiki na wanachama , na wasio natija kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa kuwapeleka kwenye miji mikuu ambako Kikwete anahubiri blah blah zake.
   
 5. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  nani kasema wanatumia hela za chama, hata kama ni hela ya chama ila kikwete yeye bado ni Rais kwahiyo bado anatumia dola, nimeona jana kwenye video akiwa mwanza na msafara wa polisi je tuone kama slaa naye atapewa msafara huo.. JK bado anaendelea kutumia gharama za serekali kwa namna moja au nyingine..
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mfumo wa serikali yetu bado ni mbovu,bado tuna shida ya kutenganisha shughuli za siasa na za serikali,ilitakiwa rais atumie gharama za chama na si serikali hata kama bado anaongoza nchi,hii inachangia sana kuvishinda vyama vya upinzani kwani wanakuwa hawana nguvu za kushindana na aliye madarakani kutokana na kuwa wakati kampeni zinaendelea wengine bado wanakuwa wanatawala.
  Kwa mtindo huu mageuzi ya kisiasa katika nchi hii ni ndoto.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na hawa Wahindi mafisadi hawana mchango kabisa katika jamii ya Watz walio katika hali ngumu au matatizo -- kama vile afanyavyo Mzee Mengi.
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Katiba Katiba Katiba..... Katiba bado ni ya chama kimoja...
   
 9. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  KKinachokera zaidi ni ile gari ya Ikulu land cruiser mpya kupakwa rangi ya kijani!
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  tizama mabango yanavyoenezwa nchi nzima, unaweZa kukuta huo ni mchango wa outdoor kwa chama, nasikia Dar makampuni yenye matangazo ya outdoor, wameombwa waruhusu ccm kutumia mabango yale kwa kampeni,
  wahindi wanasaidia ccm hata kama hawapendi, wanasaidia ccm ili waweze kupata favour katika mambo yao ya kifisadi.
  mwaka 2005 nilikua natoka Dodoma wakati JK akiwa pale Morogoro, nikiwa njiani nikapishana na abood bus 5 hivi zinatoka dumila, Magore, Tuliani , Gairo na Dakawa, nikaambiwa zimebeba wanachama na mashabiki wa ccm kwenda Moro mjini kuhudhulia kampeni za kikwete, ili kuonyesha umma namna gani anaugwa mkono.
  ule ulikua mchango wa Abood kwake, leo Aziz amepitishwa kugombea Ubunge.
  na Ikumbukwe akiwa pale Moro , Kikwete mwaka huo alipoa offer ya mafuta ya bure ya magari matano ya kampeni katika mizunguko ya nchi nzima kutoka kwa wamiliki wa TIOT.
  UTAONA MISAADA HIYO NI KILA ANAPOKWENDA, WANAFICHA MAMBO YAO.
   
 11. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mind you, usije ukadondoka itakapotokea kwamba Dr. Slaa ndiye anaingia magogoni this time around!

  Inatuuma ndio kwa sababu ni fedha za wananchi walalahoi maskini wanaodhulumiwa na wasanii wanaoitumia vibaya magogoni.
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu hili tatizo uliliona hata chaguzi zilizopita? au umeliona katika kipindi cha JK tu. Na huo mfumo umeanzia kipindi cha JK tu? Ulishawahi kuongea huko kabla ya JK? If not, MIJITU MINGINE BANA. AGHAA!
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Utakaposhan gaa zaidi pale watu ambao hata hawana credentials za kufanya kazi wanatueliwa kuwa ma-DC kulipa fadhila za kumpigia kampeni, na waliotoa fedha zao kukisaidia chama wanapewa uwaziri au tenda nyeti.
   
 14. v

  vuvuzelaorigina New Member

  #14
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa kazi yao ni kuchonga tu.walitaka Rais apande bajaj?
   
 15. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mwanahalisi limeandika Picha zake za mabango zimelipiwa na serikali yetu, sasa unategemea nini, TUNALIPA SISI KWA KODI ZETU GHARAMA ZA KAMPENI ZA CCM.
   
 16. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Nani yule wa ManU?
   
 17. M

  Malembeka Shija Member

  #17
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "wewe mbaguzi halafu hayawani....mengi anakuibia hela kwenye mfuko wako wa kushoto na kukuwekea kwenye mfuko wa kulia halafu anapata ma million ya hela kwenye mashirika.ana waalika walemavu wachache na kuwalisha pilau kwa mwaka mara moja.Hao wahindi ndio wanaoendesha uchumi wa nchi kwa viwanda na kila kitu pamojana kuongoza kulipa kodi kwa wingi.sisi waswahili tumekalia maneno na ubaguzi ambao umepitwa na wakati.waswahili wanasema UZA NYUMBA ILI UWEKE HESHIMA BAR NA NDIO TUMEJAALIWA MENTALITY HIYO.wewe ukipewa million100,basi zitaishia bar,kuhonga wanawake na kununua vogue...baada ya 6 months hauna kitu!......by pb
   
 18. M

  Malembeka Shija Member

  #18
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ndio hayawani kweli....so ukiona land cruiser yoyote unajua ni ya ikulu!hiyo ni gari ya chama na sio ya ikulu.wewe inakuuma nini?hata kodi unalipa wewe?sikazi hata tairi ya baiskeli hauna
   
 19. M

  Malembeka Shija Member

  #19
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe unavyosema fedha za walalahoi na maskini what do u mean???kama ni maskini wanapataje hela na zinafikaje serekalini???kodi inayotegemewa ni tra ambae u have to have an income na that applies kwa wale wenye hela.....u make me sick!ndio mnakalia unafik na umbea.si bora mkaimbe taarab na hama q.....by pb
   
 20. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bobby pole kwa maumivu ila ni jambo la kawaida kuumia pale unapoona jambo la kuumiza tena hasa mahali ambapo huna maelezo ya kutosha.Ni vizuri pia umeomba kujuzwa katika jukwaa hili.Safari afanyazo JK katika kampeni zake zimeandaliwa na chama chake katika kitu ambacho kila chama kinacho,namaanisha "mkakati wa kampeni na ushindi".Ndani ya hili kuna fundraising,kuna savings (kumbuka CCM imekuwepo toka 1977,kwa taasisi kuwa na akiba si jambo la ajabu),michango ya wanachama na mapato toka miradi ya chama.Hivi vyote vinakipa chama nguvu ya kusonga mbele kikampeni.Katika nchi kama Ghana,labda tu nikukumbushe kwamba hata waziri wa serikali anaporesign bado anabaki kuwa former member of cabinet.Kama mtu wa aina hii alifanya kazi vizuri,uwezekano wa kupata support ya umma kifedha na kimkakati hadi kupata ushindi ni mkubwa.Kupata vyema ninalosema jaribu kufikiri bila kadi ya chama mfukoni,it will affect ur judgement.
  Mungu Ibariki Tanzania.
   
Loading...